Mabadiliko
aliyoyaleta Imam Hussein (a.s) ambayo alikubali kuuwawa yeye pamoja na kizazi
chake,pamoja na watoto wake pamoja na wanawake aliokuwa nao, msiba huo mkubwa
uliomkumba kwaababu ya kuleta mabadilko,
Mabadiliko
hayo makubwa yalikuwa ni kuiteneneza jamii,jamii aliyoihi ilikuwa ni jamii
iliyokuwa na mapungufu mengi mno akatoka na akakubali yeye auwawa pamoja na
wanawe kwa ajili ya jamii ibadilike.katika mabadiliko makubwa aliyopambana nayo
Imam Hussein(a.s) ni kuwa na mabadilioko ya umoja,
Watu
walikuwa wamepoteza kuwa kitu kimoja, Imamu husein (a.s) akakubali afe yeye na
wanawe ili jamii alipokuwa anaishi ikamatane na kitu kinachoitwa umoja,na mimi
naamini ya kwamba matembezi haya ya amani yaliyoko leo katika mkoa wa dare s
salaam na ambayo yako katika nchi za wailamu husuani wailamu wa dhehebu la shia
ithnasheriya.
Naamini ya
kwamba matembezi haya yatakuwa ni chachuya kuwaleta watanzania waislamu kwanza
kuwa kitu kimoja wenyewe kwa wenyewe lakini pili matembezi hayo yatakuwa chachu
ya watanzania wote kuwa kitu kimoja.
Imam Husein (a.s) katika mambo amabyo alitoka kwa ajili yake na akafa kwa ajili
yake ilikuwa ni kutetea uwanadamu ni kutetea utu,
Leo
ninaamini yakwamba dunia inahitajia utu,leo naamini ya kwamba si Tanzania tu bali mahala popote pale
dunianai wanautafuta utu wa mwanadamu urudishwe, kwa hivyo naaminiya kwamba
matembezi haya ya amani huzuni hii tuliyokuwa nayo itakuwa ni chachu kubwa mno
katika ardhi ya Tanzania kuhakikisha utu unarudi katika ardhi ya watanzania,
Watanzania itakiuwa
ni sababu ya husein huyu itakuwa sababu kubwa ya sisi kutokubaguana, itakuwa ni
sababu kubwa ya sisi kupendana na kuelewana, kwahovyo ninaamini ya kwamba imam
Hussein(a.s) anahitajika leo katika ardhi ya Tanzania ,
Imam Hussein
(a.s) moja katika malengo yake na katika maelekezo yake makubwa mabadiliko yake
makubwa ilikuwa ni amani iliyopotea wakati wake imesambaratika, Hussein
akakubali yeye na watoto wake wadogo wauwawe wengine wenye chini ya umriwa
miezi 6,
kwanini kwa
sababuya kuboresha amani , utulivu na maelewano kwa wakati ule.ninaaminiya
kwamba dunia leo umegubikwa na machafuko, kila mahala vita, makundi ya magaidi
naamini ya kwamba vilevile Tanzania nayo inauhitajia utulivu, inahitajia amani,
na inahitajia mshikamano.
Naamini
yakwamba matembezi haya ya amani leo yaliyotoka katika nchi hii ya Tanzania
yatakuwa ni chachu ya kuboresha amani tuliyokuwa nayo katika nchi ya tanzania matembezi haya ya
amani yatakuwa ni chachu ya kuboresha umoja na mshikamano na mashirikiano
yaliyoko kati watanzania amabao hawabaguani dini zao hawabaguani rangi zao
hawabaguani kabila zaowatanzania wote wanakusanywa na lugha yao ya Kiswahili,
wanapendana wanaelewana na wanashikamano, wakristo waislamu hawabaguani kwa
dini zao, bali wanaheshimiana na kupendana,
Naamini
yakwamba matembezi haya yatazidi kuiboresha Tanzania kuwa kisiwa cha amani kuwa
mji wa maelewano, kuwa taifa amabalo watu wake wanapigiwa mfano kwa kupendana
na kwa kushirikiana na haya ni mafunzo tunayoyapata katika msafara wa imam
Hussein (a.s) mjukuu wa mtume Muhammad (s.a.w.w). Poleni kwa msiba wa Imam
Husein (a.s).
Na:Sheikh
Hemed Jalala
Kiongozi
Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania.
Matembezi ya
Amani, Siku ya Ashura, 01/10/2017.
Kuanzia
Ilala Boma hadi Kigogo, Dar e salaam.
No comments:
Post a Comment