Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema imeinasa
ndege isiyo na rubani ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko kaskazini
mwa Ukanda wa Gaza, ikiwa ni droni ya pili kunaswa na harakati hiyo ya
muqawama katika kipindi cha miezi miwili.
Vyombo vya habari vimeripoti
kuwa wanamapambano wa tawi la kijeshi la Hamas Izzuddin al-Qassam
waliikamata droni hiyo baada ya kuanguka katika eneo la Beit Lahia
kaskazini mwa Gaza.
Mnamo mwezi Julai, harakati wa muqawama ya Hamas
ilitangaza kuwa droni ya utawala wa Kizayuni wa Israel imeangukia huko
kaskazini mwa Gaza na kuongeza kuwa wanamapambano wa harakati hiyo
wamefanikiwa kuitengeneza ndege hiyo isiyo na rubani.
Utawala wa
Kizayuni umekuwa ukizitumia mara kwa mara ndege zisizo na rubani
kukusanyia taarifa za kijasusi katika eneo la Ukanda wa Gaza ambalo
limewekewa mzingiro wa kidhalimu wa kijeshi na kiuchumi na utawala huo
ghasibu tangu mwaka 2007.
Tokea mwaka 2008 hadi sasa utawala wa Kizayuni
umeshaishambulia kijeshi Gaza mara tatu, ambapo katika vita vya siku 50
vya mwaka uliopita Wapalestina wasiopungua 2,140 wakiwemo watoto 557
waliuliwa shahidi, mbali na 11,100 waliojeruhiwa na wengine 170,000
waliobaki bila makaazi.CHANZO IRB
No comments:
Post a Comment