Makumi ya wanamgambo ambao wampatiwa upya mafunzi na muungano wa
Marekani unaodai kupambana na matakfiri wa kundi la Daesh wameingia
nchini Syria wakitokea Uturuki.
Shirika la Haki za Binadamu la
Syria(SOHR) limeripoti kuwa wanamgambo 75 wameingia kaskazini mwa Syria
siku chache zilizopita wakiwa kwenye msafara wa makumi ya magari yenye
silaha nyepesi na zinginezo.
Rami Andulrahman Mkurugenzi wa shirika hilo
la haki za binadamu la Syria amesema kuwa wanamgambo hao waliopewa
mafunzo kwenye kambi moja karibu na mji mkuu wa Syria wailiwasili katika
mji wa Aleppo nchini Syria kati ya juzi isuki na jana asubuhi.
Mpango huo wa kutoa mafunzo kwa makundi ya wanamgambo unaoongozwa na
Marekani nchini Uturuki, uliasisiwa mwezi Mei mwaka huu lengo likiwa ni
kuwapa mafunzo wanamgambo 5400 wanaotajwa kuwa wenye misimamo ya wastani
ili kutekeleza kile kinachotajwa na Washington kuwa ni vita dhidi ya
kundi la Daesh huko Syria.
Mwezi uliopita, Walid al Muallem Waziri wa
Mambo ya Nje wa Syria aliilaumu Marekani kwa hatua yake ya kutofautisha
makundi ya kitakfiri yanayopigana dhidi ya serikali ya Damascus na
kusema kuwa, Kwa wao huko Syria, hakuna kitu kama hicho eti wapinzani
wenye misimamo ya wastani na kinyume chake na kwamba yoyote anayebeba
silaha dhidi ya serikali ya Syria ni gaidi.
No comments:
Post a Comment