Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli
akihutubia mkutano wake wa kampeni kwenye uwanja wa Chato wialayani
Chato mkoani Geita ambapo amewaomba wananchi wa Chato ambako ndiko
alikozaliwa kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika
uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Dk. Magufuli amesema mara
atakapochaguliwa serikali yake itakuwa ni ya Watazania wote bila kujali
vyama vyao, Dini zao, Makabila yao wala Itikadi zao atakuwa rais wa
watanzania wote na lengo lake kubwa ni kuwatumikia watanzania na
kuangalia zaidi na kuboresha hali za watanzania masikini ili nao waweze
kukua kiuchumi.
Dk. Magufuli amesema kuna watu
wameanza kuwatisha wananchi kwamba yeye ni mkali, Amesema “Si kweli yeye
ni mpole sana ila nikiwa madarakani nitaongoza nchi kwa utawala wa
sheria na kuwapa haki watanzania kulingana na sheria za nchi
zanavyoelekeza kuendesha nchi hivyo sitakuwa kiongozi dikteta kama
wanavyofikiri wengine”. Japokuwa ninauchukia uzembe kazini, Wizi na
ufisadi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-CHATO) |
No comments:
Post a Comment