Wakati shule zote za umma na binafsi
zikianza kufungwa kuanzia hii leo nchini Kenya, Rais wa nchi hiyo Uhuru
Kenyatta akihutubia taifa hilo kwa njia ya televisheni amesisitiza kuwa
serikali ya nchi hiyo haina uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara
wanayodai waalimu wanaoendelea na mgomo.
Ametoa wito mgogoro huo kutatuliwa kwa amani na kusema kuwa shule zote zinafungwa kuanzia leo. (Hotuba yake kamili ipate hapa,
Kenyatta: Hatuwezi kuwalipa walimu)
Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu ukiendelea.
Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za umma na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi nyumbani.
Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.
Katibu
Mkuu wa chama cha walimu nchini humo KNUT ameambia BBC kuwa tayari
amepokea barua hiyo ya kufungwa kwa shule kutoka kwa serikali.
Amesema
chama hicho kilikuwa kimeishauri serikali ifunge shule "zamani".
Mahakama inatarajiwa kuamua Ijumaa ijayo iwapo mgomo huo wa walimu,
ambao umelemaza masomo muhula wa tatu, ni halali au la. Mshirikishe
mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenza.chanzo bbc-swahili
No comments:
Post a Comment