Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran imekanusha madai ya kipropaganda yanayoenezwa na vyombo vya
habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa Tehran imelipa silaha
kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema kuwa, madai
hayo ya Wazayuni kwamba silaha za nchi hii zimepatikana mikokoni wa
Daesh katika Peninsula ya Sinai nchini Misri hayana msingi na yametolewa
kwa nia ya kuficha ukweli wa mambo kuhusu uhusiano wa utawala huo
bandia na matakfiri wa Daesh.
Uhusiano wa karibu wa Daesh, Saudia na Israel |
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, dunia
imezinduka na kila mmoja anafahamu kuwa, kundi la kigadi na kitakfiri la
Daesh linapokea misaada ya moja kwa moja kutoka nchi za Magharibi na
utawala haramu wa Israel, ikiwemo misaada ya kifedha na silaha.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran imesisitiza kuwa, sera na
misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu dhidi ya makundi ya kigaidi yakiongozwa
na Daesh iko wazi na daima taifa hili limekuwa mbioni kukabiliana na
harakati za kigaidi.
Wanachama wa Daesh katika eneo la Sinai, Misri |
Kadhalika taarifa hiyo imeongeza kuwa, dunia nzima sasa inafahamu
uhusiano kati ya Daesh, utawala wa Kizayuni, Marekani na Saudi Arabia na
kwamba ni wazi sasa walimwengu wanajua kundi hilo la wakufurishaji
lilibuniwa ili kuzusha hofu, kuvuruga amani na kusababisha ukosefu wa
usalama na uthabiti sio tu katika eneo hili bali kote duniani.Miezi kadhaa iliyopita, jeshi la Misri lilianzisha operesheni kubwa
katika maeneo ya Rafah, Sheikh Zuweid na al Aris huko Sinai Kaskazini
kwa lengo la kuyatokomeza magenge hayo ya kigaidi.Chanzo.parstoday
No comments:
Post a Comment