Sunday, June 11, 2017

Waislamu watakiwa kuwahurumia walemavu na wasiojiweza-Sheikh Abdi

Naibu Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhammad Abdi akiongea na Waandishi wa Habari katika hafla ya Futari ya Pamoja iliyofanyika Majid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.
WAISLAMU nchini wametakiwa kuishi karibu na jamii husasan kuwakumbuka watu wenye ulemavu  katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhani.
 
Mbali na hilo, wametakiwa kuwa na moyo wa kusamehe na kuwafariji watu wenye ulemavu ambao wanahitaji maalum.

Wito huo uliotolewa jana wakati wa hafla ya futari ya pamoja na watu wenye ulemavu ilioandaliwa na msikiti wa Ghadir, kigogo Post, Dar es Saalam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhammad Abdi, alisema ili dhana ya uislamu ikamilike ni lazima kuwa karibu na jamii kwa kuijali kwa kuiongezea amani na furaha.

“Uislamu si kufanya ibada tu bali ni kuitazama jamii tunayoishi ni kwa namna gani tunaijali, tunaishinayo kwa amani jambo kubwa ni kuhakikisha tunaipatie amani jamii yetu”alisema
 Image may contain: 2 people, people smiling
 Aliongeza kuwa katika vitabu vya Quran aya nyingi zinazungumzia kufunya ibada na kufunga lakini nusu ya Quran hiyo inazungumzia namna ya kuishi karibu na jamii.

NaibNaibu Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Muhammad Abdi alisema miongoni mwa mambo ambayo vitabu hivyo vitukufu vinaonesha ni namna ya kuwajali watu na kwamba hiyo ndio hali ya uislamu.

“Mtu ambaye anayempendeza Mungu ni yule ambaye anawafariji watu wengi zaidi na kwamba mbele ya Mungu hakuna mkamilifu wala mtu bora  wote ni sawa hivyo ndugu zangu walemavu karibuni hapa na mjisikie nyumbani”alisisitiza.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kigogo, George Manyama, alisema katika bajeti ya serikali ya mwaka huu imewakumbuka watu wenye ulemavu kwa kuwaondolea kodi vifaa tiba.

Alisema kinachosubiriwa ni utekelezaji wa bajeti hiyo na kwamba ni fursa kwa watu wenye ulemavu kuhakikisha wanapata mahitaji yao yote maalum katika sekta ya afya.

“Mimi ni Mwenyekiti wa kamati ya watu wenye ulemavu katika manispaa ya kinondoni hivyo ni wakati mzuri kuwataarifu kuwa kuna pesa zinatolewa na manispaa kwa ajili ya watu wenye ulemavu kuondokana na hali ya umaskini na kaunza kujikimu”alisema.

Diwani huyo aliongeza kuwa katika fedha zilizotolewa na manispaa hiyo ni zaidi ya sh.milioni 32 kwa ajili ya vikundi 36 ambapo kati yao wapo watu wenye ulemavu.

Manyima alisema miongoni mwa changamoto katika utoaji fedha hizo ni upungufu na kwamba licha ya manispaa kupeleka fedha hizo katika benki kwa ajili ya mikopo kwa watu wenye ulemavu bado kuna masharti magumu ya kukopeshwa.

“Ninashukuru uongozi wa msikiti huu kwa kuwajali na kuwathamni watu wenye ulemavu kwa kuwashirikisha katika mkusanyiko wa pamoja kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kuwafariji ambapo misikiti mingi  hawafanyi hivi kama mskiti huu nasema nashukuru sana” alisema.
 
Naye Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi wilaya ya Kinondoni, Mussa Geuza, alisema hafla hiyo inasaidia kuwakutanisha watu wenye ulemavu na kutambuana.

Alisema watu wenye ulemavu wanachangamoto kubwa ikiwemo kujaliwa na kuthaminiwa na kwamba idadi kubwa wananyanyapaliwa na kwa utaratibu ambao wanaofanya uongozi wa msikiti huo ni lakuungwa mkono.

Image may contain: 2 people, crowd
Hawa ni baadhi ya Walemavu mbali mbali waliohudhuria katika Futari ya Pmoja iliyofanyika Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam
“Hii ni fursa kubwa kwa sisi kutambuana na kufahamu taarifa rasmi kuhusu watu wenye ulemavu katika maeneo tunamoishi hivyo ninashukuru sana uongozi wa msikiti huu”alisema.

No comments: