Hali ya Mvua katika jiji la Dar es salaam.athari ya mafuriko:baadhi ya nyumba za watu zikiwa zimezingirwa na maji |
Maulana Sheikh Hemedi Jalala: Imam wa Masjid Ghadiir Kigogo Post-Dar es salaam |
Katika khutba ya leo ijumaa tarehe 8/5/2015, katika masjid Ghadiir
–kigogo Dar es salaam, Maulana sheikh Hemedi Jalala amewataka waislaam,
waumini na jamii kwa ujumla, kuwasaidia na kuwaenzi watu waliokumbwa
na mafuriko,
alisema: ” sehemu kubwa ya Jiji la Dar es salaam
limekumbwa na mafuriko na mvua kubwa, zilizosababisha baadhi ya watu
kupoteza maisha na wengine kukosa makazi na malazi, ni wajibu wetu
kuwasaidia , kwa sababu ni ndugu zetu,na jamaaa zetu, tufahamu yakua
tukio lolote linalotokea duniani lina maagizo ya mwenyezi mungu”.
Maulana aliendelea kusema, “kuwasaidia waliopatwa na matatizo ni katika
ibada, ibada ni tukio lolote linalomkurubisha mtu na mungu, kuondoa
adha, miba, chupa, misumari njiani, ni ibada , navilevile kuwasaidia,
kuwapa pole,
kuwatembelea na kutoa misaada ya kihali na mali na
kuwafariji ni ibada kubwa.ukitambua kuna mtu anamatatizo, shida ,
mitihani, fanya haraka kuyatatua matatizo yake, kwani mwenyezi mungu
ana sema fanyeni haraka kutaka msamaha wa mwenyezi mungu.”
No comments:
Post a Comment