Wanawake wakimlilia Imam Hussein (a.s) aktika siku za ASHURA. |
Hapana shaka kwamba kuwalilia wafu Waumini ni jambo
linalofaa katika Uislamu kutokana na dalili ya kitendo cha Mtume (s.a.w.w)
kuhusu jambo hilo.
Siku Mtume (s.a.w.) alipozuru kaburi la mama yake
Bibi Amina, alilia kiasi cha kuwaliza watu waliokuwa karibu yake, siku
alipofariki ami yake na mlezi wake Bwana Abu Talib, siku alipouawa kishahidi
ami yake Mtume Bwana Hamza katika vita ya Uhud
Siku alipofariki Bwana Ibrahim ambaye ni mtoto wake
mwenyewe Mtume (s.a.w.w). Mtume (s.a.w.w) alimlilia mwanawe huyu kiasi ambacho
kilimfanya Bwana Abdurahman bin Auf amwambie Mtume (s.a.w.w): "Na wewe
unalia Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu"? Bwana Mtume (s.a.w.w) akasema:
"Ewe mwana wa Auf hiyo ni alama ya huruma".
Alipotimia Imam Husein umri wa miaka miwili Mtume
alitoka kufanya safari na katika safari yake hiyo alisimama mahali fulani, basi
aliamua kutoendelea na safari yake na mara macho yake yakawa yanabubujika
machozi, akaulizwa sababu gani iliyomfanya alie. Mtume (s.a.w.) akasema:
"Jibril ananieleza kuhusu ardhi iliyoko kando
ya mto Furat iitwayo "KARBALA" mahala ambapo atauawa mwanangu Husein,
sasa hivi ni kama nauona uwanja wa mapambano baina yake na adui zake, pia kama
kwamba napaona mahala atapozikwa.
Kisha baadaye Bwana Mtume (s.a.w.) aliamua kurudi
hali ya kuwa mwenye huzuni na majonzi, akapanda katika Mimbari na akatoa khutba
huku Hasan na Husein (a.s.) wakiwa mikononi mwake.
No comments:
Post a Comment