Taarifa zinasema kuwa mazungumzo ya kusaka amani kati ya pande hasimu
za Sudan Kusini yanakwamishwa na hatua ya serikali ya Juba ya kukataa
takwa la kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa.
Mabior Garang msemaji wa ujumbe wa waasi ulioko Addis Ababa Ethiopia amesema kuwa, haijaelezwa wafungwa hao vipi wataachiliwa huru na jambo hilo ndilo ajenda kuu ya mazungumzo.
Ameongeza kuwa, ana wasiwasi upande wa serikali unatumia kadhia hiyo ya wafungwa kukwamisha mazungumzo ili uweze kujipatia ushindi kwenye medani ya vita.
Msemaji wa ujumbe wa serikali ya Sudan Kusini Michael Makuei amesema, serikali ya Juba haijakataa takwa hilo lakini imezigawa ajenda katika sehemu mbili, na hivi sasa wanajadili jinsi ya kumaliza uhasama na baadaye watajadili kadhia ya wafungwa.
Katika upande mwingine askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamefyatua risasi na kuwatawanya wapiganaji waliokuwa karibu na kituo cha umoja huo cha Malakal, baada ya watu waliokuwa na silaha kuingia kwenye kituo hicho ambapo makumi ya wakimbizi walijeruhiwa na mmoja kuuawa.
C hanzo irib

No comments:
Post a Comment