Tuesday, January 14, 2014

Imarati yataka Iran iondolewe vikwazo

Umoja wa Falme za Kiarabu umesifu makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya Iran na madola sita yenye nguvu duniani na kutaka kuondelewa vikwazo dhidi ya Tehran.

Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu amesema kuwa Iran ni jirani ya Imarati na pande zote zitanufaika iwapo jamii ya kimataifa itaiondolea Iran vikwazo.

Uhusiano wa Iran na Imarati ni wenye umuhimu mkubwa kwa pande zote mbili kwa kuzingatia kuwa makumi ya maelfu ya Wairani wanaishi huko Imarati.

Nchi hiyo inatumika kama njia kwa ajili ya miamala ya kibiashara kati ya Iran na nchi nyingine za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi. 

Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alifanya ziara nchini Imarati mwezi Disemba mwaka jana ili kuboresha uhusiano na nchi hiyo jirani ya Kiarabu na mshirika wa kiuchumi.
Chanzo irib


No comments: