Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa katika viwanja vya Mnazi mmoja, jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya kukumbuka mazazi ya Mtukufu wa daraja Mtume
Muhammad (s.a.w.w)
Kuwakusanya watu kwa ajili ya sherehe ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume
Muhammad (s.a.w.w) ni kuitukuza sifa zake ambazo zimesifiwa na Mwenyezi
Mungu (s.w.t). Nabii Isa (a.s) alimuomba Mwenyezi Mungu amteremshie meza
ya chakula, na siku hiyo ya kuteremshwa meza ya chakula akaitaja kuwa
ni sikukuu: "Ee Mwenyezi Mungu Mola wetu! tuteremshie chakula kutoka mbinguni ili kiwe sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu na kiwe ishara itokayo kwako, na turuzuku, kwani wewe ni mbora wa wanaoruzuku". 5:114.
Je. thamani ya kuwepo Mtume Mtukufu, ni
ndogo kuliko meza ya chakula iliyotoka mbinguni ambayo Nabii Isa (a.s)
ametangaza siku ya kuteremshwa chakula hicho kuwa ni sikukuu? Ikiwa
kufanywa siku hiyo sikukuu ni kwa sababu chakula ilikuwa ni ishara ya
Mwenyezi Mungu, Basi Je, Mtume Muhammad (s.a.w.w) si ishara kubwa kabisa
ya Mwenyezi Mungu? Mwenyezi Mungu anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu
anamteremshia rehema Mtume, na Malaika wake wanamteremshia rehema Mtume,
enyi mlioamini! Muombeni rehema (Mtume) na muombeni amani". 33:56
iliposemwa Aya hii, Maswahaba waliuliza Mtume: Watamuombeaje rehema?
Mtume akawafundisha, semeni: Allahumma swali a'laa Muhammad wa Aali
Muhammad.
No comments:
Post a Comment