Rais Barack Obama wa Marekani ametishia kupiga kura ya veto
muswada wowote wa vikwazo vipya dhidi ya Iran wa Baraza la Seneti la
nchi hiyo wakati huu ambapo Jamhuri ya Kiislamu na nchi za kundi la 5+1
zinapojitayarisha kuanza kutekeleza makubaliano ya nyuklia ya Geneva.
Obama amesema katika taarifa yake ya maandishi kwamba kuweka vikwazo vipya dhidi ya Iran kutahatarisha juhudi za utekelezaji wa makubaliano ya mwezi Novemba mjini Geneva.
'Nitapiga veto muswada wowote wa vikwazo vipya dhidi ya Iran katika kipindi hiki cha mazungumzo ya kundi la 5+1 na Iran', amesisitiza Obama na kuongeza kuwa hatua kama hiyo inaweza kukwamisha juhudi za kutatua kadhia hii kwa amani.
Muswada wa vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Iran umetayarishwa na Seneta wa chama cha Republican Bob Menendez.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza kuwa haiwezi kufanya mazungumzo chini ya vitisho na mashinikizo na kwamba iwapo Marekani itapasisha vikwazo vipya hatua hiyo itakuwa na maana kuwa makubaliano ya nyuklia ya Geneva yamekufa.
Chanzo.irib.ar
No comments:
Post a Comment