Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa wanaomba dua ya Umoja baada ya Swala ya Ijumaa.
Habari Kamili
Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam Dhehebu la Shia
Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalala amesema Kama Mashia na Masuni wakikaa
pamoja katika kujadili maendeleo ya Uislam, mafanikio makubwa yatatokea.
Hayo
ameyasema leo katika Khutba ya Swala ya Ijumaa ya pili ya Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani 1436, sawa na 26/06/2015, ikiwa ni ramadhani ya 9.Ila kasisitiza kwa
kuacha tofauti tulizokuwa nazo.
Mawlana Sheikh Jalala amesema Ramadhani ni Madrasa kubwa
sana inayotufundisha Umoja, Ummoja wa watu na Waislamu kwani Moja ya jambo
linalofurahisha ni kufaradharishiwa watu wote kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.
“Moja ya falsafa ya kufaradhirishiwa watu waliopita
na walioopo kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani ni swala la umoja.Ibada ya mwezi
wa ramadhani unatufundisha kusahau tofauti zetu na kuwa na jambo moja katika
jamii yetu”amesma Sheikh Jalala.
Amesema Mtume alipoingia madina kitu cha kwanza
alichokifanya ni kutengeneza umoja,Umoja uliokuja kutengenezwa na Mtume kati ya
Muhajirina na Aswar ndio iliyotengeneza Serikali ya Kiislam Darasa la ramadhani
inatufundisha kuacha tofauti zetu na kuwa kitu kimoja.
Hatahivyo amesema Waislam ndio waathirika wakubwa
katika umasikini uliokithiriMadrasa ya ramadhani ni kuondoa matatizo katika
jamii, bila ya kuacha tofauti zetu hatutofikia malengo ya Ramadhani.
|
No comments:
Post a Comment