Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akihutubia Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam |
Na ndio
maana tunapong’ang’ania kwamba sisi Watanzania jambo la Uongozi linatukusanya
sisi sote kama Watanzania pasina tofauti za dini zetu, na wala waislam wasije
wakaja wakadhania kuna siku watakuja kuwabadilisha watanzania wote wawe waislam
hiyo haitotokea hata siku moja na wala ndugu zetu Wakristo wasije wakaja
wakadhania kuna
siku
watatuhubiria sote tukamuacha Muhammad Ibn Abdillah (s.a.w.w) na tukamfuata
Yesu (a.s) haitotokea,kwahiyo kilichobakia ni sisi kuvumiliana ndani ya nchi
moja na kama dungu wamoja.
Kumbe mwisho wetu Nabii Issa / Yesu (a.s) ataswali
nyuma ya Imam Mahdi (a.s).Malengo ya Nabii Issa / Yesu (a.s) na malengo ya Imam
Mahdi (a.s) ni mamoja ni kuijaza dunia amani, maelewano, masikilizano na
mshikamano.
Na.Sheikh Hemed Jalala
Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia
Ithnasheriya Tanzania
#KhutbayaIjumaa2016
No comments:
Post a Comment