Friday, September 23, 2016

“Inashangaza jamii ya Kiislam hakuna Hospitali na Shule zinazotoa huduma Bure” Sheikh Swalehe

Sheikh Abdullatif Swaleh akizungumza jambo katika maadhimisho ya Eid al Ghadir, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam
“Ni jambo la Kushangaza katika jamii yaWaislam kuna Hospitali nyingi yako chini ya Waislam lakini ni Binafsi, lakini sijawahi kuona kuna Hospitali kwamba hii Hospitali ni ya Waislam wote katika hii Tanzania yetu, Sijui kuna Hospitali ambayo ni maalumu Kuwa Hospitali hii ni ya Waislam,

Mwislam anaenda kutibiwa bure,mwislam anatatizo lake,vipimo anaenda kupimwa bure, ikiwa inahitajika tiba anatibiwa bure, Waislam wote tukitaka tujue ni majanga ya namna gani tunayokabiliana nayo kutokana na ukosefu wa kuwa na Uongozi, tena Uongozi imara,uongozi madhubuti, 

uongozi wenye hekima  busara na utambuzi ya kinifu unaojua kwamba ni jambo gani linaloendelea katika ulimwengu,na sisi kama wa wanajamii ya jamii Fulani kama Waislam tunahitajika tufanye nini?

Waislam hatuna Hospitali, Waislam hatuna Shule ni Waqf kwa Waislam kiasi kwamba Mwislam yeyote angienda kusoma bure hatuna, lakini tuna Shule za watu binafsi, hivi tujiulize wale watu binafsi wanapesa nyingi kuliko sisi Waislam wote pindi tukiunga na jibu ni hapana, lakini kukosekana Uongozi katika jamii ndio sababu inayopelekea kukosekana huduma hizo katika jamii.ndio sababu iliyopelekea kukosekana huduma hizo katika Jamii”Sheikh Swalehe.

Sheikh Abdullatwif Swalehe
#Eid al #Ghadir2016

No comments: