Wednesday, June 1, 2016

Kila mwananchi ahifadhi na kutunza vyanzo vya maji pamoja na kupanda miti-Mushi

Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Raymondi Mushi ametoa wito kwa kila mwananchi kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji pamoja na kupanda miti kwa maeneo anayoishi.

Amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari katika Uzinduzi wa kuadhimisha siku ya mazingira Duniani ,Dar es salaam na kuwahimiza Wananchi kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kufanya usafi katika maeneo yote ya makazi na biashara.

Aidha Mushi amewatahadharisha wakazi na wananchi wote amabao ni wachafunzi wa mazingira kuacha mara moja kwani atakayekiuka taratibu za usafi na kusababisha uchafuzi wa mazingira atachukuliwa hatua za kisheria.
Mh Mushi amewahimiza Wakandarasi wanaotoa huduma ya uzoaji taka katika wilaya ya Ilala kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya kutosha na kutoa huduma inayokidhi mahitaji kwa wananchi.

Hatahivyo Mh Mushi ametoa wito kwa kila mkazi wa Halmashauri ya Ilala kushiriki kikamilifu kwa pamoja katika wiki hii hadi tarehe 5 ambapo ni kilele cha kuadhimisha siku ya mazingira Duniani.

No comments: