Muhandisi Heri Hatibu wa Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi, akisisitiza jambo. |
Muhandisi Heri Hatibu amesema Wakala wa Taifa wa
Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi wameanza kazi za Utafiti, ushauri na
ukandarasi katika kuwapatia wananchi wa Tanzania nyumba na makazi bora ya
kudumu kwa gharama nafuu hasa kwa wenye kipato cha chini.
Hayo amesema leo jiji Dar es salaam, wakati akiongea
na Wanandishi wa habari na kusema kuwa tafiti mbalimbali zimeshafanywa mojawapo
ikiwa ni utafiti kuhusu “Embodied and Operational Energy”
Muhandisi Hatibu amesema kuwa Utafiti huu utasaidia
kupunguza kiwango cha nishati kinachotumiwa kwenye nyumba kwa ajili ya kupooza
hewa na kuokoa fedha inayoweza kutumika kufanya mambo mengine.
Aidha kwa upande wake Muhandisi Benedict Chilla
amesema kuwa lengo la utafiti huo ni kusaidia kupunguza kiwango cha hewa ya
Ukaa inayotolewa kwenye shughuli zinazohusiana na ujenzi na kusaidia kupunguza
uharibifu wa mazingira.
Muhandisi Benedict Chillawa Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi |
Hatahivyo nae Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na
Masoko ndugu Zubeda Salum amesema kuwa wadau wa sekta ya ujenzi waelimishwe
kuhusu nishati na mazingira ili sekta ya ujenzi ifanyike kwa kuzingatia
maendeleo endelevu.
Muhandisi Heri Hatibu Wakala wa Taifa wa
Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi, pembeni yake ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Masoko ndugu Zubeda Salum |
No comments:
Post a Comment