Monday, May 8, 2017

Sheikh Jalala atoa pole, awataka Wazazi wafiwa kuwa na subira na Uvumilivu kwa kuwapotea watoto wao Wanafunzi wa Lucky Vicent, Arusha

Kiongozi Mlkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania akitoa salamu za polena rambirambi kwa msiba wa wanafunzi 32 wa lucky Vicent leo Majid Ghadie,Kigogo Post Dar es salaam.
Kikao na Waadishi wa Habari, Kimechofanyika leo, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam, Msiba wa Wanafunzi 32 pamoja na Walimu, Wa shule ya Lucky Vicent, Mkoani Arusha.

Kwa jina la Mwenyezimungu mwingi wa Rehema mwenye kurehemu.

Innalilah Wainna lilah Rajiiun
Sisi sote tumetoka kwa Mungu na sisi sote mwisho tutarudi kwa Mungu.

“Tumepokea kwa masikitiko makubwa na kwa huzuni ya hali ya juu, isiyokuwa na kifani, ajali ya basi ya shule ya Lucky Vicent ya mjini Arusha iliyotokea katika eneo la mrima Rotia, Karatu na kusababisha vifo vya baadhi ya wanafunzi waiopungua 32 ikiwemo baadhi ya walimu,

Sisi kama Watumishi wa Imam Swadiq (a.s) makao makuu yapo hapa Kigogo Post Dar es salaam, sisi kama Waislamu, vilevile sisi kama waislamu wafuasi wa madhehebu ya Shia Tanzania tunaungana na watanzania wenzetu wote  waslamu na wakristo wanaoishi Tanzania kutoa mkono wa Pole kwa wazazi, kwa wanafunzi wote waliofiwa,na uongozi mzima wa shule ya Lucky Vicent na wanafunzi wenzao ambao bado wapo shuleni hapo.
 Image may contain: 4 people, people sitting and camera
Na vilevile tunatoa mkono wa pole kwa taifa letu takatifu kwa ujumla na vilevile tonatoa pole kwa muheshimiwa Raisi wa Taifa hili la Tanzania Dr. John Magufuli.

Napenda kusema hili limetugusa kwa dhati kama waumini, kama watanzania, kwasababu tunaposoma katika quran ndio kitabu chetu waislamu, inatuambia yakwamba “Waumini wote ni ndugu”  kwahivyo lililotokea limewakumba waumini wenzetu,ni wajibu wetu kama watanzania pasia kubaguana  kidini,  kiitikadi kimadhehebu,kupendana kuelewana na kuwa pamoja wakati wote waraha na wakati wa majanga kama hili limetukumba  katika kipindi hiki.
 Image may contain: 1 person, sitting and on stage
Mtume Muhammad (s.a.w.w) anaema; hakika sifa ya waumini wanatabia ya kupendana na kuhudhumiana  kama vile unavyoona mwili mmoja,  kiungo kimoja kinapougua na viuongo vingine vinakesha kwa kuugua haviwezi kubakia salama salmini.

Mwisho Mungu awape wafiwa subira uvumilivu, na wote waliotangulia mbele ya haki Mungu wapokee roho zao kwa mikono miwili na awaweke mahala pema  ndani ya pepo takatifu, na sisi tuliobakia hapa nchini Tanzania Mungu atupe upendo, atupe mshikamano, atupe umoja, atupe kuvumiliana, atupe kuenzi amani na utulivu tuliokuwa nao , Mungu ibariki Tanzania wabariki watu wake wote  wabariki viongozi wake, amiin amiin amiin,Asateni sana.

Imetolewa na
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala

No comments: