Monday, May 8, 2017

“Amani, maelewano na masikilizano kwa watu wenye Dini zote Tanzania lazima itunzwe kwa hali yoyote” Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiwasilisha mada yake mbele ya hadhira katika Ukumbi wa Nkurumah, University of Dar es salaam, jijini Dar es salaam.
   Na Twalah Ndiholeye

Amani ya Mwenyezimungu iwe kwenu
Semina “Dini na Maadili  ya Ubinadamu Ulimwenguni”
Ukumbi wa Nkurumah, Univesity of Dar es salaam.
06/05/2017

Semina hii imeyowekwa mahala hapa Chuo Kikuu malengo yake makubwa ni malengo ya kumuangalia Mwanadamu, madhumuni makubwa ni kuangalia nafasi ya mwanadamu, katika maisha ya kila siku, na vile vile malengo makubwa  ya Semina hii kuwekwa katika ardhi ya Tanzania katika Mkoa wa Dar es salaam,

Bila shaka leo hii duniania inakabiliwa na Vita vya wenyewe kwa wenyewe, dunia inakabiliwa na kukosa amani, dunia inakabiliwa namauaji ya kinyama, dunia inakabiliwa na matatizo ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya kuumbwa mwanadamu.

Na kwa bahati mbaya yanayotokea leo hii wakati mwingine yanatokea kwa jina la dini, yanatokea kwa jina la Uislamu,kwamba anaefanya ni Mwislamu, yanatokea  anaefanyiwa ni Mwislam, vilevile kwa hivyo malengo makubwa ni kutaka kuleta mwanga na kuleta maelekezo, ya kwamba dini zote ikiwemo dini ya Uilamu, zikiwemo dini ya Ukristo pamoja na Uyahudi, dini zote malengo yake makubwa ni kukaa vizuri na mwanadam, 

malengo yake makubwa ni kuleta amani, malengo yake makubwa ni kuleta mshikamano, malengo yake makubwa ni kuleta kuvumiliana katika jamii, ya watu wanaoishi wenye mitazamo tofauti, na fikra tofauti na rai tofauti kuweza kukaa pamoja, ndio malengo makubwa ya kutumwa mitume wote mnaowatambua, ndio malengo ya makubwa ya vitabu vya mwenyezimungu vyote vilivyotoka minguni,kwanzia taurati,injiri, zauri mapaka kufikia Quran tukufu,

Nukuta ya pili kwanini semina hii yenye lengo ya mwanadamu wote kumtengeneza mwanadam,kumnyosha mwanadamu katika hali ya Tanzania,  Mtakubaliana namimi ya kwamba Tanzania imekuwa ikijulikana katika historia  ni kisiwa cha amani, Dar es salaam, ukijulikana ni mji wa amani, Tanzania imekuwa na sifa tofauti na nchi zingine, Tanzania inasifa ya watu wake wanaishi katika amani, inasifa  watu wake hawajui kubaguana kidini, kimakabila,kimadhehebu, 


na kifikra ,
Watanzania wamekuwa wakikaa pamoja bila ya kubaguana, kwa aina yeyote, bali hadi makabila yao hawajuiani wakati mwingine, inawakusanya pamoja lugha ya Kiswahili.
Kwahiyo semina kama hii kufanywa katika sehemu kama hii ya Tanzania ni kutoa maelekezo na kutoa funzo kwa vijana haswa,

 kwamba utulivu huu, busara hii, hekima hii, kukaa huku pamoja kwa watu wenye dini zote lazima kuweziwe, lazima kubakishwe, lazima watu wafanye bidii yoyote inayowezekana hali kama hii ya utulivu iweze kuendelea. Aanteni sana.

Imetolewa na
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala

No comments: