Katibu wa Jumuiya ya Vijana BAKWATA Sheikh Othman Zuberi akizungumza leo Masjid Ghadir, Kigogo Dar es salaam juu ya Umuhimu wa Sensa na kumpongeza Mh. Muft wa Tanzania Abubakar Zuberi. |
“Kama umoja
wa Vijana wa Kiislamu BAKWATA Taifa tunaomba kuwatoa hofu wale wote ambao
wanaoona zoezi la Sensa, kwa Wiaslam linaweza kugeuka kuwa chanzo cha mfarakano
wa Taifa Kiimani, haiwezi kuwa hivyo tunavyomfahamu Mhe. Muft wetu Abubakkar Zuberi ni mwenye
kuongozwa na Qur’an na hadith za Mtume Muhammad (s.a.w.w)” alisema Katibu wa
Umoja huo Sheikh Zuberi
Sheikh
Zuberi amesema kuwa dhima kubwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa Waislamu
wanahesabiwa, makatibu wanapaswa kumsaidia mufti katika hilo ili kuweza kuwa na
Idadi kamili ya Wailsamu hapa nchini na kufahamu wako wapi, wanafanya nini,
wangapi hawana kazi, wazee wangapi, nguvu kazi ikoje taarifa ambazo ni muhimu
kwa mustakabali wa Waislamu.
Akizungumza leo Jijini
Dar es Salaam katika eneo la Masjid Al Ghadir Kigogo Post, Katibu wa Jumuiya ya
Vijana BAKWATA Sheikh Othman Zuberi alisema tangu alipochaguliwa Muft Abubakar
mwaka 2015 ameweza kufanya mambo mbalimbali baada ya kutoa maelekezo kwa
viongozi wa dini ikiwemo kudumisha amani, kuunganisha jamii, kuleta
maendeleo, ushirikiano mzuri wa Baraza na Mashirika ya Dini ya ndani na nje ya
nchi.
Aidha Sheikh
Zuberi ameendelea kusema kuwa Mh.Muft kaamrisha mema na kukataza maovu,
uboreshaji wa elimu ya dini na secula, kusisitiza kujitambua, mahusiano mazuri
kati ya Baraza na viongozi wa nchi, kukataza kufanya kazi kwa mazoea, na sensa
kwa maendeleo ya waislamu ambapo ameagiza kupatikana kwa takwimu sahihi kwa
waislamu kupitia misikiti mbalimbali hapa nchini.
Hata hivyo Sheikh
Zuberi ameongeza kuwa Mh. Muft katika kuonyesha umakini Mkubwa katika
kuwatumikia Waislamu, hivi karibuni aliwaagiza makatibu wa Baraza la BAKWATA
kujiandaa na Sensa ya waislamu, Misikiti na Madrasa kote nchini, ni zoezi lenye
lengo jema la kutoa huduma kwa usahihi kwa watu unaowatumikia.
Waandishi wa Habari, Vijna wa Umoja wa Kiislamu BAKWATA Taifa na baadhi ya wageni waliohudhuria katika kikao hicho kutoka Chuo cha Kiislamu (Hawzat) Imam Jafar Swadiq (a.s) wakifauatilia kwa ukaribu jumbe mbalimbali zinazotolewa na Umoja huo, leo Masjid Ghadir, Kigogo Post, Dar es salaam. |
No comments:
Post a Comment