Umoja wa Katiba ya
wananchi UKAWA leo ameitaka Tume ya taifa ya uchaguzi kutoa tamko kuhusu kauli
iliyotoleawa na mmoja wa viongozi wa CCM kuwa chama hicho hakipo tayari
kuondoka ikulu hata kama kitashindwa katika uchaguzi ujao mwaka huu.
Kauli hiyo ilitolewa katika
kampeni za Urais mkoani kigoma na mmoja kati ya viongozi wa chama hicho ndugu
ABDALA BULEMBO ambapo alisema kuwa hakuna njia inayoweza kuwaondoa ikulu na
chama cha mapinduzi hakiwezi kuachia IKULU kwa njia yoyote kauli ambayo imeanza
kuibua mijadala mbalimbali nchini Tanzania.
Akizungumza na
wanahabari mchana wa leo mwenyekiti wa chama cha Democrasia na maendeleo
chadema ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa UKAWA ndugu FREMAN MBOWE amesema
kuwa kauli hiyo imewashtua sana wao kama vyama vya upinzani na kuanza kuwa na
wasiwasi kama uchaguzi huo utakuwa na amani kwa kuwa chama chenye serikali
kimeapa kufanya njia yoyote ili tu kisiachie ikulu.
Mh MBOWE amesema kuwa
kauli hiyo inaweza kuchukuliwa kawaida lakini ni kauli nzito na yenye mafumbo
makubwa ambayo yanaweza kusababisha vurugu kubwa na hadi sasa hakuna mtu yoyote
wa chama hicho wala tume ya uchaguzi aliyejitokeza kutolea ufafanuzi kauli
hiyo.
Amesema kuwa kama kauli
hiyo ni kauli ya chama cha mapinduzi ni ukweli kuwa vyama vya upinzani
havitaweza kuwa na imani na uchaguzi huo kwa kuwa tayari chama tawala kimesema
hakiko tayari kuachia ikulu huku akienda mbali na kusema kuwa kwa kauli hizo
hakuna haja ya kuendelea kuwa na uchaguzi ambao chama tawala kinangangania
ikulu.
Mh MBOWE amesema sasa
UKAWA unaitaka tume ya taifa ya uchaguzi kukitaka chama cha mapinduzi kutolea
ufafanuzi kauli hiyo kwani kama ndio kauli yao watangaze kabisa kuwa hakuna
uchaguzi kwa kuwa utakuwa ni upotevu wa rasilimali za taifa wakati tayari chama
tawala hakiko tayari kukubali matokeo..
MGOGORO WA NCCR
MAGEUZI.
Aidha katika hatua
nyingine mwenyekiti huyo wa chadema amesma kuwa sakata linaloendelea ndani ya
chama cha NCCR MAGEUZI ni mwendelezo wa baadhi ya viongozi wa vyama hivyo
kuendelea kufika bei ya kutaka kuisaliti ukawa na hakuna lingine.
Hivi juzi viongozi
kadhaa wa chama cha NCCR waliibuka na kudai kuwa chama chao kimekuwa kikiyumba
kutokana na mwenyekiti wao kufanya kazi za chadema kuliko za chama huku wakidai
kuwa wamekosa majimbo mengi ambayo walikuwa wanayatarajia ambapo Mh mbowe
amesema kuwa hiyo sio hoja kwani lengo la UKAWA sio chama kuwa na majimbo
mangapi bali ni kuhakikisha kuwa wanaibuka na majimbo mengi bila kujali vyama
vyao.
Mh mbowe amesema kuwa
swala la mgawanyo wa vyama lilienda sambamba na kuangalia uwezo wa chama husika
katika jimbo na kusimamisha mtu ambaye anakubalika katika eneo husika ili
kuweza kupata ushindi katika majimbo mengi na sio kutoa majimbo hata kwa watu
ambao hawakubaliki katika majimbo hayo.
No comments:
Post a Comment