Sheikh Muhammed Abdi akizungumzia tukio la Eid al Mubahala Masjid Ghadir, Kigogo Post, Dar es salaam |
“Kwanini
wewe unaitikadi kuwa upo katika haki, upo katika njia sahihi uogope kumsogelea
mwingine, kwanini huyu anaesema yeye yuko sawasawa aogope kwenda kuwasikiliza
Mashia Ithnasheriya, hii ni yaleyale kipindi cha Mtume Muhammad (s.a.w.w)
Makuraishi wa makka walikuwa wakiwakataza watoto wao , vijana wao wasiende
kumsikiliza Mtume Muhammad (s.a.w.w) Yule ni mchawi,akizungumza yale maneno
yake yanavutia na ushawishi ,hii ni kuonesha udhaifu.
Udhaifu wa
hoja, udhaifu wa itikadi ya Imani, udhaifu kwa kile ambacho wanakiamini lakini
aya hii inasema la (suratul al Imran aya 58-61) sisi itikadi yetu ni dhabiti,
ndio maana bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuonesha itikadi yake ni dhabiti
aliwambia njooni, hajasena msije.
Na sisi
tunawambia wale wote ambao wanasema kwamba Ushia Ithnasheriya sio sahihi,
tunawambia njooni,njoni Kigogo,njooni Masjid Ghadir, mwenye hoja tutampa
mimbari
azungumze,tumsikilize na tumuulize maswali, na sisi tupo tayari watwite
twende tuzungumze, watuulize maswali, hiyo ndio hoja, hayo ndiomazungumzo,
hivyo ndio watu wanatakiwa wakae Yule ambae atashindwa basi akishindwa na
akiona ameshindwa lakini hataki kufuata basi atakaa pembeni lakini mzungumzo
yatakuwa yameisha”
Na.Sheikh Muhammed Abdi
#Eid al #Mubahala2016
No comments:
Post a Comment