Baraza Kuu la chama cha CUF limemtimua uanachama aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kuanzia leo.
Katika
kikao chake kilichoongozwa na Mbunge wa Tandahimba, Katani Ahmed Katani
kimepitisha uamuzi huo leo baada ya kuungwa mkono na wajumbe wote 43
waliohudhuria kikao hicho.
Mashtaka dhidi ya Limba yaliandaliwa na
Sekretarieti ya chama yakimtuhumu kufanya vurugu, kuharibu mali za
chama na kudharau barua ya wito wa chama kwenda kujitetea.
Mwishoni
mwa wiki Lipumba aliongoza mashabiki wake kuvunja geti na milango ya
ofisi ya chama hicho, Buguruni Dar es Salaam baada ya kutengua uamuzi
wake wa kujiuzulu, hatua iliyoungwa mkono na Msajili wa vyama vya siasa,
Jaji Francis Mutungi.
No comments:
Post a Comment