Maulana Samahat Sheikh Hemed Jalala akiwaswaisha kwa Vitendo waschana waliohudhuria katika kusherekea kuzaliwa kwa Bibi Zaynab Bint Ali.
Hawazat Imam Swadiq imesheherekea mazazi ya Bibi
Zaynab Bint Ali (a.s) kwa kuwachukua
wasichana 50 wenye umri wa miaka kuanzia 9 hadi 15, pamoja na wazazi wao kwa
kuwapatia elimu na mafunzo juu ya Unuhimu wa Hijabu, Swala na sheria zingine za
Kiisalamu.
Katika Mafunzo hayo, Samahat Sheikh Hemed Jalala
aliwasalisha swala ya jamaa kwa vitendo na kuwataka waschana hao waishi kwa
misingi ya Kiislamu,na Wapambike na hijjab kama walivyokuwa Fatma Bint Muhammad
(s.a.w.w) na Zaynab Bint Ali (a.s)
Bibi Zainabu Baba yake ni Sayyedina Ali Ibn Abutwalib (a.s), Mama Yake ni Fatuma Bint
Muhammad, Babu yake ni Muhammad Ibn Abdallah na Bibi yake ni Khadija Bint
Khuwailid
|
No comments:
Post a Comment