Sheikh Hemed Jalala,akisisitiza jambo juu ya Uislam Sahihi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). |
Sheikh Hemed Jalala, Kiongozi wa Chuo cha Kiislamu
kilichopo Kigogo-Post, jijini Dar es Salaam amewataka Waislamu kufuatilia
Uislamu halisi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa Makini katika kusikiliza jumbe mbalimbali kutoka kwa Wahadhiri. |
Hayo ameyasema katika Mhadhara wa Wazi uliokuwa wa siku tatu kuanzia 28, februal, hadi 01-machi 2015, katika viwanja vya Super Sanifu, Round About ya Kigogo, Dar-es -salaam.
Amesema kuwa Uislam wa
Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni uislamu wa Amani, kuvumiliana, kupendana, kuheshimiana,
kutokukufurishana ,kutodharau dini ya mwenzio na Wenyekukaa Pamoja na watu
wenye mtazamo tofauti.
Aidha ameongeza kuwa Uislamu wa Mtume ni wa amani, huruma na
maelewano na kuwa Uislamu halisi utashinda Uislam wa chinja chinja utafeli
kwa kuwa unaenda kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu (s).
Hatahivyo amewataka
watu wote bila kujali dini zao kushikamana na kusikilizana kwani jamii ambayo
aina maelewano itakuwa ipo mbali na maendeleo, taifa ambalo linapata maendeleo
ni taifa lenye maelewano na mshikamano.
Katika Muhadhara huo uliyomalizika siku ya J.pili ya tarehe 1/03/2015 kulitolewa vitabu mbalimbali vinavyoonesha athari mbaya ya Madhehebu ya Kiwahhabi (ANSWARU SUNNA) Madhehebu ambayo hii leo yamekuwa tishio kubwa kwa jamii ya Kiislamu Ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment