Waaumini wa Dini ya Kiislam na Wapenda Amani Duniani wakitembea ktika Matembezi ya Amani ya Siku ya Kimataifa ya Quds,leo Dar es salaam |
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnsheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amewataka watanzania kuunga mkono harakati za kupinga vitendo
vya dhuruma na unyanyasaji vinavyofanywa dhidi ya wapalestina.
Kiongozi Mkuu wa Wislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Wndishi wa Habari katika Mtembezi ya Amni ya Siku ya Kimataifa ya Quds.leo Dar es salaam. |
Amesema ikiwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa ambayo yanasifika kuwa
ni kisima cha amani hivyo ni wajibu wa kuipigania amani kwa nchi
zingine ambazo imetoweka.
Sheikh Jalala amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika matembezi ya amani
ya kuwakumbuka wapalestina ambao wamepoteza amani waliokuwanayo,
matembezi hayo yalioanzia Ilala Boma hadi Viwnj vya People Kigogo jirani na Msjid Ghadir, Dar es salam
Sheikh Jalala, amesema kuwa kuna haja ya kuhakikisha watanzania wanafanya
juhudi za makusudi za kupinga vitendo vinavyoendelea nchini Palestina
ili nao wae na amani kama iliokuwa awali.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiongea na Waandishi wa Habari katika Matembezi ya Amani ya Siku Kimataifa ya Quds |
Amesema Tanzania ina kila sababu ya kupinga vitendo hivyo kutokana na
kuwa hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alikuwa kiongozi wa taifa
alipinga hali hiyo ya vitendo vinavyofanywa dhidi ya wapalestina.
“Mwalimu Nyerere alikuwa karibu na wapalestina katika kudai haki yao
hivyo bado Tanzania inatakiwa kuunga mkono juhudi zilizoanzishwa na
mwasisi wa taifa katika kudai hali ya amani nchini humo”alisema.
Wanawake wa Kiislam na Wapenda Amani Duniani wkishiriki katika Matembezi ya Amani ya Siku ya Kimataifa ya Quds yaameyofanika leo Dar es salaam |
Siku ya Kimataifa y Quds ni siku ya kuwakumbuka Wapalestina na Watu wote ulimwenguni wanaoonewa, Siku ya Kimatifa iliasisiwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Imam Khomein (r.a), ambae aliteua Siku ya Kimatifa ya Quds kuwa kila siku ya Ijumaa ya Mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment