Habari Kamili
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, amewataka viongozi wa dini kutokuwa
na ubaguzi na badala yake kuwapigania wanyonge ili kupata haki zao.
Aidha,
amewasihi viongozi hao kujitoa kama Imam Khomein (r.a) ambaye alijitoa
kwa ajili ya watu wote ulimwenguni na kwamba hakujitoa kwa ajili ya waislamu
pekee wala Mashia, bali alijitoa kwa wanadamu kupata haki zao.
Wito
huo ulitolewa jana Dar es Saalam wakati wa semina iliyozungumzia mchango
wa Imam Khomein (r.a) katika ulimwengu, ambayo iliyofanyika katika Masjid
Ghadir, Kigogo Post Dar es Salaam.
“Historia
haiwezi kumsahau Imam Khomein (r.a) bali ni lazima tuendelee kumkumbuka kwa
sababu ni Kiongozi ambae ni mfano katika jamii, kwani alilingania umoja, haki,
usawa na alipinga kila aina ya unyanyasaji na dhuluma katika jamii” alisema
Sheikh Mussa.
Aidha,Sheikh
Mussa alisema Imam Khomein (a.s) ni Kiongozi ambae ni mfano katika jamii kuna
haja ya kuigwa mazuri yake na kwamba si bali alikomboa Mapinduzi ya Kiislam ya
Iran, lakini pia alifanya mapinduzi ya kifikra.
“Imam
Khomein (r.a) aliwakomboa watu waliodhulumiwa, alisimamia haki na
uadilifu katika jamii,kuhakikisha mnyonge anakuwa na haki duniani,’’alisema.
Muanzilishi na Kiongozi wa Kanisa la Ufunuo Tanzania Nabii Paulo Bendera akiongea katika semina hiyo. |
Kwa
upande wake Kiongozi wa Kanisa la Ufunuo Tanzania, Nabii Paulo Bendera, alisema
amejifunza mambo makuu matatu kutoka kwa Imam Khomein (r.a) ambayo ni usawa,
haki na kuwatetea watu wanaonyonywa na wanaokandamizwa katika jamii.
Alisema
Imam Khomein (a.s) alikuwa ni mtu wa watu, alikuwa anapenda haki, usawa na
aliwatetea watu wanaonyonywa pamoja na kuwatumikia watu kwa moyo wa dhati,
“Nashukuru
sana kwasababu ninajifunza mengi ndani ya dini ya Kiislamu, hata miezi
iliyopita nilimkaribisha sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kanisani kwangu
na nikampatia fursa ya kuhutubia na waumini walifurahi sana”alisema
Aliongeza
kuwa viogozi wa dini wanapaswa kuonyesha ushirikiano baina ya viongozi wa
Kikristo na wa Kiislamu na kwamba ni wajibu kufungua nafasi zaidi ya upendo,
mahusiano mema kati ya wakristo na waislamu.
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea katika Semina hiyo. |
Naye
Kiongozi Mkuu wa madhehebu ya waislamu wa Shia, Ithnasheriya Tanzania
Sheikh Hemed Jalala alisema kuwa uislam unatoa mafunzo ya kuishi vizuri na watu
wote, pamoja na kuwa na moyo wa huruma.
No comments:
Post a Comment