Sunday, February 10, 2019

Uzinduzi wa Kitabu cha Shirazi na Baluchi kinaonyesha Uhusiano kati ya Tanzania na Iran

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mhe. Mousa Farhang akifanya Uzinduzi wa kitabu cha Shirazi na Baluchi kinachoonyesha kwa Uwazi Historia ya Tanzania na Iran, 08.02.2019, katika Ukumbi wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jijini Dar es salaam.

Na: Twalha Ndiholeye
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mhe. Muosa Farhang amesema kuwa kitabu cha Shirazi na Baluchi ni kitabu kinachoonyesha Uhusiano wa wazi na wa kihistoria kati ya Taifa la Tanzania na Taifa la Iran.

“Leo hii tunafuraha kubwa kwa uzinduzi wa Kitabu ambacho kinaelezea historia ya Washirazi, Wabaluchi na Watanzania, kwa kuzingatia kwamba uwepo wa Washirazi na Wabaluchi katika Tanzania kulikuwa na athari kubwa kwa vizazi vijavyo” Balozi Farhang.

Balozi Farhang alisema hayo jana baada ya Uzinduzi wa Kitabu hicho kilijulikanacho kwa jina la Shirazi na Baluchi, uzinduzi huo ulifanyika katika kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jijini Dar es salaam.

Aidha Balozi Farhang aliwataka Watnzania kuwa na uwelewa sahihi juu ya uhusiano wa wazi na wa kihistora katika ya Taifa la Tanzania na Taifa la Iran kwa kupitia Shirazi na Baluchi ambao walifika Tanzania kabla hata ya Uhuru wa Tanzania na kuwa makini na wale wote wanaopotosha Historia hii.

“Uzinduzi huu wa Kitabu hiki ni sehemu tu ya utamaduni na historia amabyo inabidi watanzania waelewe, na ninaamini itabaki kwa muda mrefu,Napenda kuwaambia watanzania kuna historia ndefu na kubwa zaidi ambayo iliyopita, ila nasikitika hii historia inaanza kupotea ambapo inadini sasa historia ianzwe kurudiswa, bila shaka historian a utamaduni mkubwa walionao watanzania inaweza kusaidia nchi zote za jirani, eneo la afrika mashariki” alisema Balozi Farhang

Kwa Upande wake Muadishi wa kitabu cha Shirazi na Baluchi Mhe. Charles Kayoka alisema kuwa kitabu hiki cha Shirazi na Baluchi kinaonyesha Shirazi na Baluchi waliingia nchini kabla ya miaka 300 kwa Baluchi na 1000 kwa Shirazi iliyopita.

“Kitabu hiki kinazungumzia kwa ufupi historia ya Wabalunchi na Washirazi kama watu ambao walikuja nchini zaidi ya miaka 300 wabalunchi na zaidi ya miaka 1000 kwa upande wa Shirazi”

Charles Kayoka ambae pia ni Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika Idara ya Sanaa na Ubunifu alisema kuwa Kiatabu kinaonyesha Ushahidi wa kuja kwao kwa ushahidi wa majumba na ushahidi wa watu ambao wameshakuwa viongozi au nyumba za makazi ambayo waliwahi kuishi maeneo mbalimbali, Picha za makazi ya watu na watu wenyewe zilitoka afrika mashariki kama Mtwara, Lindi, Unguja na Pemba nchini Zanzibar, Tanga pamoja na Mombasa.

“Hichi kitabu kwa sisi watanzania kinajaribu kuonyesha ni Taifa ambalo linahistoria ndefu na pana, ambayo inatakiwa ichapishwe, nap engine kuangalia namna gani historia hii itaendelea kutafitiwa zaidi, kwa ajili ya kuiboresha historia yetu, ambapo kwa wale walioandika kunavitu vingi waliviacha, hii itatusaidia sisi kama Watanzania”


No comments: