Viongozi wa
dini mbalimbali na serikali wametakiwa kuwa karibu na vijana ili
wafundishwe maadili mema wasije kuwa na
fikra za ugaidi baada ya kukata tamaa ya
kukosa kazi.
Wito huo
ulitolewa jan Dar es Salaam na Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithanasheriya
Tanzania, Sheikh Hemed Jalala, katika futari ya pamoja na vijana hao wa kiislam na wasiokuwa waislamu wa Kata ya
Kigogo wakati akizungumza nao kutambua
lengo la uwepo wao.
Hawa ni baadhi ya Vijana wa Kiislam na Wasiokuwa Waislamu wa kata ya Kigogo waliohudhuria katika Futari ya pamoja iliyofanyika Majid Ghadir, Kigogo Post Dar es alaam. |
Sheikh
Jalala, alisema vijana wa sasa wamejitenga na mambo ya kiroho wamekata tamaa ya
maisha kwa kukosa kazi hivyo ni wajibu wa viongozi kuwa karibu nao kusikiliza
changamoto zao.
"Vijana ni tunu ya taifa, ndio muhibili wa jamii kwani taifa ambalo halina
vijana wenye maadili mazuri liko hatarini kuwa na vijana ambao wanaweza
kujiingiza na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na ugaidi.
Sisi kama
viongozi ni wajibu wetu kuwa karibu nao kuwafundisha namna ya kuwa karibu na
nyumba za ibada ili baadaye tuweze kuwa na vijana watakaoliendesha taifa letu
la Tanzania,’’alisema.
Mwl. Kassim Hassan ambae pia ni Mdau wa mambo ya Kijamii kutoka shule ya Sekondari Kibondo akiwapa elimu vijana walioudhuria semina jana Kigogo jijini Dar es salaam. |
Alisema
vijana watakapokuwa wamefundishwa kwamba
Mungu ni mpenda amani na kinachokubaliwa
ni maelewano mazuri na sio ugaidi.
Hatahivyo Jalala, alisema dini ya kiislam haina
mahusiano na masuala ya ugaidi ambayo ni kuuana na kuchinjwa kwani Uislam
inafundisha Amani,mshikamano na maelewano kwa kila mtu.
Hawa ni baadhi ya Vijana wa Kiislam na Wasiokuwa Waislamu wa kata ya Kigogo waliohudhuria katika Futari ya pamoja iliyofanyika Majid Ghadir, Kigogo Post Dar es alaam. |
No comments:
Post a Comment