Kiongozi
Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala
amesema kuwa moja ya lengo la kufanya Matembezi ya Amani ya Kukumbuka Mazazi ya
Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni ishara ya Huruma tuwenayo Binadamu Tanzania na
Dunia kwa Ujumla.
“Matembezi
haya ya Amani ya kukumbuka Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni ishara ya
Huruma ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuweza kuieneza katika mitaa yetu na Sehemu
zetu na Tanzania kwa ujumla, kwani Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliletwa kwa watu
wote na sio kwa watu Fulani tu” alisema Sheikh Jalala
Sheikh
Jalala alisema hayo jana katika Matembezi ya Amani (ZAFA) YA Kukumbuka Kuzaliwa
kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu T.I.C pamoja
na Hawzat Imam Swadiq Kigogo Dar es salaam.
Sheikh
Jalala alisema kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) anafundisha huruma kwa watu wote
bila kujali tofauti za dini,tofauti za madhehebu, tofauti za Kifikra na Kimtazamo,
na tofauti za Rangi na Taifa.
“Mitaa hii
ya Kigogo imejaa watu wenye dini tofauti, watu wenye madhehebu tofauti, watu
wenye mitazamo tofauti, watu wenye rangi tofauti, matembezi haya ya kukumbuka
kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni kumuunga Mkono Mtume Muhammad (s.a.w.w),
kwamba yeye aliletwa kwa ajili ya watu wote”.
Aidha
ametataka Viongozi wa dini ya Kiislamu, Kikristo, Wanasiasa na Viongozi wa
Serikali kujenga mazoea ya kuwatembelea Wananchi wao bila kujali tofauti za
hali ya Kimaisha pamoja na Kipato walizonazo wananchi wao kwani kufanya hivyo
ni kumuenzi mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.w).
“Matembezi
haya ya kukumbuka kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni ishara ya waziwazi ya
kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliingia Mitaani, kukutana na watu, kukutana na
watu wa kawaida, kukutana na watu amabo sio matajiri na wala sio watu wenye
uwezo mkubwa, malengo makubwa ni kuwaleta watu pamoja na kuwafanya watu wote
kuwa kitu kimoja bila kuwabagua dini.”
Kwauapande
wake Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu ya Shia Ithnasheriya Tanzania
(T.I.C) Sheikh Ramadhani Mwelekwa amewataka Watanzania kuendelea kuwa na Umoja
na Mshikamano kwani kufanya hiyo ni kuenzi Mafundisho ya Mitume wa Mwenyezi
Mungu akiwemo Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Nabii Issa/ Yesu Kristo.
“Waislamu
wote na wale hawajabahatika kuwa waislamu tumeungana kwa ajili ya kuonyesha
Umoja na mshikamano ambao ndio lengo la kutumwa Mtume Muhammad (s.a.w.w),
tunafurahiya wote bila kujali itikadi zetu za kimadhehebu na wale ambao
mnatuona Mitaani lengo kubwa ni kufikisha Ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)
kwa watu wote na Ulimwengu wote
No comments:
Post a Comment