Naibu Mkuu
wa Hawzat Imam Swadiq (a.s) Sheikh Muhammad Abdu amewataka Viongozi wa Dini kuhamasisha Vijana
kushiriki katika Michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa Mpira wa Miguu, kwani
inapelekea Amani katika maeneo yetu tunayoishi pamoja nan chi kwa ujumla.
“Lakini
vilevile ni mchezo unaoweza kuleta amani, katika maeneo yetu, leo tuko hapa
mambo mengi huko mitaani yamesimama, kama mtaa wetu una vibaka, vibaka wote
wako hapa, kama kuna wezi wote wako hapa, inamaana mambo yote machafu
hayafanyiki.” Alisema Sheikh Abdu.
Sheikh Abdu
alisema hayo jana katika Fainali ya Lingi ya Mtume (s.a.w.w) Cup, kwa kukumbuka
kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), uliochezwa katika Viwanja vya Pipo
Kigogo Post Dar es salaam.
Sheikh Abdu
ambae pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya Waislamu T.I.C amesema
kuwa Michezo ni katika mafundisho ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake pale ambapo
Uislamu unasema Mwislamu mwenye nguvu na mwenye Mazoezi anapendwa zaidi mbele
ya Mungu kuliko Mwislamu dhaifu ambae hana nguvu na hafanyi mazoezi.
“Na hii
inatupa picha kwambaMichezo sio tukio linalofanywa na watu pengine ni wahuni au
ni watu ambao hawana Kazi,Tukio la Michezo ni tukio hata watu wa dini
wanatakiwa walitile nguvu na walifanye kwasababu ni moja katika maamrisho Mungu
na vilevile ni mafundisho ya Uislamu kwamba, Mwislamu mwenye nguvu na mwenye
Mazoezi anapendwa zaidi mbele ya Mungu kuliko Mwislamu dhaifu ambae hana nguvu
na hafanyi mazoezi” Alisisitiza Sheikh Abdu.
No comments:
Post a Comment