Kiongozi
Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala
amewataka Wanafunzi wa Dini ya Kiislamu wahubiri Umoja, Upendo, mahusiano
mazuri na utulivu pindi wanapokuwa wamemaliza masomo yao.
Maulana
Sheikh Jalala amesema hayo katika Kikao na Waandishi wa Habari ikiwa ni katika
kukaribisha kumbukizi ya Mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w),iliyofanyika jana
masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam.
“Tumewaomba
wale ambao wamemaliza Masomo yao katika chuo hiki, Seminari hii ya Imam Swadiq
(a.s) waende wakalinganie Umoja wa watanzania, waende wakalinganie Upendo wa
watanzania, waende wakalinganie mahusiano mazuri ya watanzania, waende
wakawalinganie watu wakae vizuri katika nchi hii na kuboresha utulivu tulionao” amesema Sheikh Jalala
Aidha
Maulana Sheikh Jalala amesema kuwa kwa kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume
Muhmmad (s.a.w.w), Masjid Ghadir umejipanga kuimarisha Mahusiano mema katika ya
Kata ya Kigogo na Tanzania kwa Ujumla ili kuleta amani na Utulivu katika maisha
yetu ya kila siku.
“Mtume
Muhammad (s.a.w.w) alikuwa ni mtu wa Mahusiano Mazuri, Msikiti wa Kigogo wa
Masjid Ghadir, katika kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) umejipanga
kuhakikisha kwamba mahusiano yanakuwa
mazuri kwa watu wote wanaoishi kata hii ya Kigogo na Tanzania kwa Ujumla.” amesisitiza Sheikh Jalala
Kwauapnde
wake Mkuu wa Kituo cha Al-Mustafa Khairiya Sheikh Ali Mwazoa amewataka
Watanzania kuwa wazalendo katika kuipenda nchi yako katika kuhakikisha jamii
yako katika eneo unaloishi wanakuwa salama na Amani.
“Mtume
Muhammad (s.a.w.w) anasema kuipenda nchi yako ni katika imani” nchi inamaana ya
watu, lazima ifikie uwapende watu wan chi yako, watu wa kijiji chako, watu wa
mji wako,kuipenda nchi yako ni kuhakikisha mazingira ya nchi yako yanakuwa ni
salama na amani kwa maisha ya wanadamu na maisha ya viumbe kwa Ujumla” Amesema
Sheikh Mwazoa.
No comments:
Post a Comment