Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh
Hemed Jalala ameataka Viongozi wa Dini ya Kiislamu na Kikristo, Wanasiasa
pamoja na Viongozi wa Serikali kudumisha na Kuenzi UMOJA huu tuliyonao
Watanzania pamoja na kuwataka kutolaghaiwa tukafikiwa mahala Umoja huu
ukasambaratika.
“Jambo Muhimu tuondoke nalo, Kikao kinachoweza kuwakusanya
Waislamu Shia Ithnasheriya, AhlulSunna, Maibadhi,Wasiokuwa Waislam Wakristo,
Mayahudi hili ni jambo la kuenziwa, Waislam, Wakristo na Wanasiasa ambao mpo
katika Jukwa Kuu, tusije tukalaghaiwa, tukafikia mahala umoja huu wa
Kimadhehebu, Kidini na wa Kitanzania ambao ndio sababu ya utulivu huu unaouona
na kujivunia huku tulikokuanako ni jambo la kuenziwa na Masheikh, Maskofu,
Wanasiana pamoja na Viongozi wa Nchi” Alisema Sheikh Jalala
Sheikh Jalala alitoa wito huo jana katika Hafla ya
Kusheherekea Kumbukumbu ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambapo Mgeni
Rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo, iliyofanyika
Jana chini ya Usimamizi wa Jumuiya ya Waislamu T.I.C Pamoja na Hawzat Imam
Swadiq , Iliyofanyikia jana katika Viwanja vya Pipo Kigogo Dar es salaam.
Kwa upande wake Mhe. Ali Mkomwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya kisarawe akiongea kwa Niaba ya Mgeni Rasmi Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo aliwataka
Waislamu pamoja na Watanzania kudumisha Amani na Umoja wa Waislamu.
“Jambo la Kwanza Mhe.Waziri alichoniagiaza ni swala
la Amani, ili tuwehuru katika kufanya Ibada zetu na mambo yetu,kuna watu leo
hawapendi kuona utulivu huu uliopo, jambo la pili aliloniambia niseme ni Umoja
wetu wa Kiislamu, na kwa bahati nzuri Sheikh Alhad amelizungumza kwa upanda
sana” Alisema Mkomwa
Nae Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa
amesema Swala ya Umoja wa Kiislamu ni Jambo muhimu Sana na kuwataka Waislamu
Kushirikiana kwa yale wanayokubaliana na kwa yale hatukubaliani tusilazimishane
ambapo ndio chanzo cha uvunjifu wa Amani na Utulivu tulionao.
“Sheikh Jalala, Mimi siku zote utambulisho wangu ni wa Umoja
wa Kiislamu, sitoweza kuwa Shia Ithnasheria nitaendelea kuwa AhlulSunna, nay
eye Sheikh Jalala hawezi kuwa AhlulSunna ataendelea kuwa Shia Ithnasheriya,
Jambo la Muhimu ni Umoja wa Kiislamu kama hapa tulivyokaa, Masheikh wa
AhlulSunna na Masheikh wa Shia Ithnasheria na Watoto wetu tunamsheherekea Mtume
Muhammad (s.a.w.w), katika yale tunayokubaliana tunakuwa pamoja, tusiokubaliana
tunaachana tutakutana akhera shida iko wapi?” Alisema Sheikh Alhad Sheikh Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam.
Hatahivyo Nae Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya
Chama cha Mapinduzi Mhe. Ali Mtulia amemtaka Sheikh Jalala kuendelea kufanya
kazi za Kijamii badala ya kujikita tu katika mambo ya Dini pekee, ambapo ndio
miongoni mwa kazi alizokuwa anafanya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambae ndio
Kiigizo chetu.
“Sheikh Jalala nakushukuru sana kwa hadhara hii nzuri,
nimeonana na wapigakura wangu wa Kinondoni, lakini nikuombe Sheikh
Jalala,alikuwa Kiongozi wa Dola yake, lakini alikuwa anafanya Shughuli za
Kijamii, akikusanya zaka, wakitoa Sadaka, wakifanya mambo ya Tiba, wakifanya
Mambo ya Mahusiano, wakitoa na Ushauri, Sheikh wangu Sheikh Jalala, nakukabidhi
Kata ya Kigogo uendelee kufanya Mambo ya Kijamii” Mbunge wa Mtulia
No comments:
Post a Comment