Wakati jeshi la polisi
nchini Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es
salaam wakiendelea na msako mkali kuwasaka wale wote waliohusika na mauaji ya
askari katika kituo cha polisi cha STAKISHARI,Hatimaye mtuhumiwa mmoja ambaye alikuwa
anatafutwa na polisi kwa kuhusiaka na tukio hilo amejisalimisha makao makuu ya
jeshi la polisi akiambatana na familia yake.
Akizungumza na
wanahabari makao makuu ya jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam kamishna
wa polisi wa kanda hiyo SULEMAN KOVA amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni ZAHAQ
RASHID NGAI maarufu kama MTU MZIMA,ambapo amesema kuwa mtuhumia huyo
alijisalimisha makao makuu ya jeshi la polisi akiwa na wake zake wawili baada
ya kusambaa kwa taarifa kuwa anatafutwa kwa hali na mali na jeshi la polisi.
Katika Taarifa ya
polisi wakati wakielezea mafanikio ya polisi kuhusu tukio hilo iliyotoka terehe
20 mwezi wa saba ilimtaja ndugu ZAHAQ RASHID NGAI maarufu kama MTU MZIMA kama
mmoja wa vinara wa tukio lile .
Mtuhumiwa huyo
anayedaiwa kuwa msaidizi mkuu namba mbili wa kiongozi wa kundi hilo lililovamia
kituo cha polisi stakishari tarehe 12 mwezi wa saba anaendelea kuhojiwa na
jeshi la polisi.
Aidha katika msako wa
polisi wamefanikiwa kukamata watuhumiwa wengine wawili waliohusika na tukio
lile ambao wametajwa kwa majina kama—
1-RAMADHAN HAMIS miaka
18 mkazi wa Mandimkongo
2-OMARY OMARY AMIRI
miaka 24 mkazi wa mbagala.
Jeshi la polisi
linaendelea kuwahoji watuhumiwa hao
No comments:
Post a Comment