Raia wawili wa Tanzania waliotiwa mbaroni na polisi nchini Kenya kwa
tuhuma za kuingia nchini humo ili kusajili wasichana kujiunga na kundi
la kigaidi la Al Shabaab watapandishwa kizimbani wiki ijayo.
Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya, Joseph Nkaissery ametangaza
habari hiyo na kuongeza kuwa, Watanzania hao wawili walikamatwa kwenye
eneo la mpakani la Isebania kaunti ya Migori baada ya wananchi kutoa
habari kwa polisi.
Serikali ya Kenya mwezi huu imetoa tahadhari ya
uwezekano wa kutokea mashambulizi ya kigaidi ya al Shabaab wakati wa
mwezi mtukufu wa Ramadhan na hivyo vyombo vya usalama vimeimarisha doria
kukabiliana na hali kama hiyo.
Nkaissery pia ametuma salamu za rambi
rambi kwa nchi tano ambazo zilikumbwa na hujuma ya kigaidi siku ya
Ijumaa. Katika taarifa yake, Nkaissery amesema hujuma za kigaidi za
Ijumaa katika nchi za Somalia, Tunisia, Ufaransa ,Syria na Kuwait ni
ishara kuwa Kenya inapaswa kukaa katika hali ya tahadhari. Sambamba na
kulaani hujuma hizo za kigaidi, Nkaissery amesema Kenya inajiunga na
mataifa. Chanzo IRIB
No comments:
Post a Comment