Saturday, October 24, 2015

Sheikh Jalala “Sababu ya Kutoka Imam Hussein (a.s) ni kuienzi Amani”







 Habari Kamili
Jambo ambalo wanayo waislam wote duniani siku ya kumi au siku ya Tisa haya yanakuwa ni masiku ya Muharam, masiku haya tunakumbuka kifo cha mmoja katika wajukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). anaitwa Imam Hussein (a.s), bwana huyu Imam Hussein (a.s), ni mjukuu wa Mtume alitoka na aliuwawa katika masiku kama haya.
Lakini niseme yakwamba  kuuwawa kwa Imam Hussein (a.s)  kama mjukuu wa Mtume nadhani na Mtume Muhammad (s.a.w.w) naye vilevile amefariki, amekufa na amezikwa , kwanini mnaiona huzuni hii, watu wamevaa nguo nyeusi mnazoziona katika matembezi haya. Hayo ameyasema leo katika matembezi ya Amani ya kukumbuka siku aliyouwawa Imam Hussein (a.s),mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).yaliyo anzia Msikitini wa Kablastani hadi Jirani na Msikiti wa Khoja Shia Ithnasheriya Posta, Dar es salaam.
Swala kubwa ni Ujumbe aliokuwa ameubeba Imam Hussein(a.s), ujumbe huu naamini yakwamba ni ujumbe mkubwa , na ujumbe alioubeba, ulikuwa ni Ujumbe wa Uwanaadamu, Imam Hussein (a.s) kwenye kipindi chake ni kipindi ambacho, Uwanaadamu ulikiuwa umesambaratika , utu ulikuwa hakuna , Imam Hussein (a.s) akaja katika kumrudisha mwanaadamu, kuwa mawanaadamu anaheshima, kurudisha umoja wa Wanaadamu.
Na moja ya mambo muhimu sana ambayo ni mazuri kuyagusia haya  na ambayo Imam Hussein (a.s) hatosahauliwa hata siku moja  na ambalo Watanazania leo wanalihitajia, Imam Hussein (a.s), moja ya mambo muhimu aliyetoka kwa ajili yake ilikuwa ni kuienzi amani, ni kuenzi maelewano, ni kuenzi mshikamano, ni kuenzi kusikilizana.
Imam Hussein (a.s) ametoka kwa sababu kipindi chake watu walikuwa wanakaa pamoja , hii hali ya umoja ilikatika, hali ya maelewano ilisambaratika , hivyo akatoka na ujumbe mkubwa wa kuhakikisha kwamba  katika nchi zile amani inarudi, utulivu unarudi, busara inarudi, kuelewana kunarudi na akawa yupo tayari hata watoto wake wadogo wauwawe, lakini ahakikishe nchi inakuwa na amani,utulivu unakuwepo.
Na sisi Watanzania leo hii  tukikumbuka kifo cha Imam Hussein(a.s) moja ya jambo kubwa ambayo ndio ujumbe wetu kwa watanzania wote pasina kubagua dini zao, iwe ni waislam , iwe ni wakristo,iwe ni Mabudha na iwe watu ambao hawana dini, Watambue yakwamba moja ya ujumbe tunaoubebe ni Ujumbe wa kuhimiza amani, amani hii waliyonayo watanzania kwa miaka mingi, amani hii ambayo ni tunu la taifa letu, ni tunu ya dini, bali asili ya Dini yenyewe ni amani.
Na mimi naamini ya kwamba dini zote za mungu, iwe ni Ukrito,uwe ni Uislam,uwe ni Uyahudi, hazikuja kuleta kufarakana , hazikuja kuleta kugombana , hazikuja kuleta kuvutana. Bali zimekuja kuleta maelewano, masikilizano na amani.
Watanzania kipindi hiki cha uchaguzi watambue yakwamba kuienzi amani ndio dini, Wakristo na Waislam, walitambue hilo, na wale ambao watashindwa au watashinda, kwenye vichwa vyao waweke yakwamba  sisi watanzania ni watu tumezoea amani,ni watu tuiozoea maelewano ni watu tunaotambua Tanzania ni kisiwa cha amani, na kwamba jambo la amani ni jambo la dini, na kwa ajili ya jambo hilo Imam Hussein (a.s) ameuwawa kwa ajili yake, na leo tunalikumbuka 
Mwisho niseme yakwamba tujitokeze kwa wingi kupiga kura, kwa sababu ndio wajibu wetu wa kisheria nay ale mambo yote ambayo yataondoa amani, yataondoa masikilizano, mambo hayo ni Harram, (hairuhusiwi) kwa sisi watu wa dini kuyasogelea, na ni wajibu (lazima ) kuenzi kila jambo ambalo litahakikisha tunapiga kura , tunawachagua Viongozi, tukiwa nchi bado imetuli.
Nnchi bado ni kisiwa cha amani, na tuangalie nchi za wenzetu kwenye vitindi vya uchaguzi, kwenye vitindi vya kampeni mazingira yao ni magumu na amani yao imetoweka , amani iwe juu ya Imam Hussein (a.s) aliyetoka kwa sababu ya kuienzi, umoja na Ubinaadamu na maelewano. Asanteni sana.


Na: Sheikh Hemed Jalala, Mmoj wa Viongozi Wakuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania.

No comments: