Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala
amewataka Masheikh na wanazuoni wa Ahlul Sunna Dar es salaam na Tanzania nzima
kuungana na Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania ili waendee kuwa wamoja na
kuweza kumshinda Adui anaofanya kazi ya kuwagawa.
“Enyi Ndugu zangu,
Wasomi, Masheikh na Wanazuoni wa AhlulSunna Tanzania kuweni macho, Waislamu
Shia Ithnasheriya ndio wenzenu, na Mkitaka Usuni uwendelee, ninawaambia
Masheikh wa Ahlul Sunna wa Dar es salaam na Tanzania nzima waungane na Mashia
Ithnasheriya ndio ndugu zao na wabaki pamoja, na wakitaka wamshinde adui wa
Usuni wawe pamoja na Mashia Ithnasheriya” Amewataka Maulana Sheikh Jalala.
Maulana Sheikh Hemed Jalala amesema hayo leo Khutba ya
Swala ya Ijumaa, imeyoswaliwa wiki iliyopita, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es
salaam, ambapo katika khutba hiyo alizungumzia Je, Usuni na Uwahabi ni Kitu
Kimoja?.
Aidha Maulana Sheikh Jalala amewatahadharisha Wasoni,
Masheikh na Wanazuoni wa Kiahalul Sunna kuwa macho na gurupu linalofanya kazi
ya kuwagawa AhlulSunna na Shia Ithnasheriya kwa kutofuata maelekezo yao ambayo
inaonekana ndio chanzo cha Matatizo mengi katika jamii ya Kiislamu.
“Nataka niwaeleze Ndugu zangu, Wasomi na Wanazuoni wa Ahlul
Sunna katika nchi hii wakae wakitambua kwamba hilo gurupu linalowaambia
Waislamu Shia Ithnasheriya sio wenzenu, msiwaalike kwenye Maulid zenu,
msishirikiane nao, msiende kwenye misikiti yao, hao ndio sio wenzenu katika
Ahlulsunna, na hao ndio waliowaletea matatizo mengi” Maulana Sheikh Jalala amesema
Hatahivyo Maulana Sheikh Jalala amewatoa hofu Watanzania kwa
kusema kuwa Dini tukufu ya Uislamu asili unalingania watu kuwa wamoja,
kupendana na kutokuunga mifarakano yoyote ambayo itapekekea migogoro yoyote
katika jamii ya Kiislamu.
“Watanzania Mungu
amewaletea Uislamu ambao hauwagawi watu, unawatakeni muwe kitu kimoja,
unawatakeni mpendane, vipi linakuja gurupu linaanza kuwagaweni huyu ni Shia
Ithnasheriya na huyu ni Ahlul Sunna?,huyu ni Ibaadhi huyu ni Ghawarij?, mbona
sivyo Uislamu ulivyo?,?” Amesisitiza Maulana Sheikh Jalala
No comments:
Post a Comment