Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Duniani amesema
suala la Palestina ni la kuhuzunisha mno linalomuumiza kila mtetezi wa
uhuru, haki na uadilifu duniani.
Ayatullah
Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo hivi punde katika hotuba ya ufunguzi
wa mkutano wa sita wa kimataifa wa kuunga mkono Intifadha ya Palestina
unaofanyika hapa mjini Tehran ambapo mbali na kuwakaribisha wageni wote
waalikwa amesisitiza kuwa historia ya Palestina na kuvamiwa na kukaliwa
kwake kidhalimu kwa mabavu, kufanywa wakimbizi mamilioni ya watu pamoja
na muqawama wa kishujaa wa taifa hilo shujaa kumeshuhudia hali ya faraja
na misukosuko mingi.
Kiongozi Muadhamu amebainisha kuwa upembuzi makini katika historia
unaonyesha kuwa hakuna kipindi chochote cha historia, wala hakuna taifa
lolote duniani lililowahi kukabiliwa na mateso, machungu na hatua za
kidhalimu kama taifa la Palestina ambapo kutokana na njama iliyopangwa
nje ya eneo lake nchi hiyo ikavamiwa na kukaliwa kwa mabavu kikamilifu,
watu wake wakatimuliwa katika majumba yao na badala yao likatafutwa
kundi moja la watu kutoka huku na kule duniani na kupelekwa huko;
uwepo
halisi wa watu wa eneo hilo ukapuuzwa na badala yake uwepo bandia na wa
kubuni ukawekwa mahala pake; hata hivyo, huu pia ni ukurasa mwingine
mchafu wa historia ambao kama zilivyo kurasa nyingine chafu utafungwa tu
kwa idhini na msaada wa Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maelezo kamili ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu itakujieni katika matangazo yetu yajayo
No comments:
Post a Comment