Craig Deare, afisa mwandamizi katika serikali ya Marekani ametimuliwa kwa kukosoa sera za Rais Donald Trump wa nchi hiyo.
Deare, ambaye ni afisa mwandamizi wa Baraza la Usalama wa Taifa
ameachishwa kazi baada ya kukosoa sera za Trump na washauri wake wa
karibu.
Afisa huyo mwandamizi wa serikali ya Washington ambaye aliteuliwa
mwezi uliopita kuongoza kitengo cha baraza hilo katika eneo la
Hemisphere ya Magharibi alisindikizwa na maafisa wa usalama kutoka jengo
la ofisi aliyokuwa akifanya kazi mjini Washington.
Afisa mmoja mwandamizi wa Ikulu ya White House amethibitisha kuwa
Deare si mfanyakazi tena wa Baraza la Usalama wa Taifa na kwamba
amerejea kwenye shughuli yake ya hapo kabla katika Chuo Kikuu cha Taifa
cha Ulinzi.
Afisa huyo amethibitisha ripoti hiyo kwa sharti la kutotajwa jina lake pasina kutoa maelezo zaidi.
Hata hivyo baadhi ya maafisa wa serikali ya sasa na ya zamani ya
Marekani wamesema, Craig Deare amefukuzwa kufuatia matamshi aliyotoa
siku ya Alkhamisi iliyopita katika kikao cha faragha kilichofanyika
kwenye kituo cha tanuri fikra cha Wilson kilichoko mjini Washington.
Kwa mujibu wa mmoja wa watu waliohudhuria kikao hicho, Deare
aliishambulia vikao serikali ya Trump kutokana na sera zake kuhusiana na
eneo la Amerika ya Latini hususan kwa kuanzisha mikwaruzano na
serikali ya Mexico.
Katika wiki ya kwanza mara baada ya kuingia madarakani, Rais wa
Marekani alisaini dikrii ya ujenzi wa ukuta katika mpaka wa pamoja wa
nchi hiyo na Mexico, ikiwa ni kutekeleza ahadi aliyotoa wakati wa
kampeni za uchaguzi. Hatua hiyo ilimfanya Rais Enrique Pena Nieto wa
Mexico avunje safari yake ya kuelekea Marekani aliyokuwa amepanga
kuifanya mwishoni mwa mwezi Januari.
Imeripotiwa kuwa Deare alionyesha waziwazi kukasirishwa na kukatwa
mijadala yote ya sera kuhusiana na Mexico na kueleza kwamba washauri wa
karibu wa Trump akiwemo mkuu wake wa stratijia Steve Bannon na mkwe wa
Rais huyo Jared Kushner hawakuwasiliana na kurugenzi ya Baraza la
Usalama wa Taifa wakati serikali ilipokuwa ikiandaa sera
No comments:
Post a Comment