Tuesday, December 20, 2016

LEMA AENDELEA KUSOTA RUMANDE MAHAKAMA YA MWONGEZEA SIKU ZA KUWASILISHA KUSUDIO LA RUFAA

Image result for PICHA ZA LEMA ARUSHANa mahmoud Ahmad Arusha 
MAHAKAMA kuu kanda ya Arusha, imetoa muda  wa siku  kumi kwa upande wa utetezi wa kesi ya kumyima dhamana mbunge waArusha, Godbless Lema, kuwasilisha kusudio la kuomba kuongezewa muda wa kukata rufaa ili aweze kupewadhamana.
Uamuzi huo umetolewa leo na jaji Dakta Modesta Opiyo wakati akiamua hatima ya mbune huyo kupata dhamana au la
Jaji Opiyo amesema hoja za Upande wa serikali zilizowasilishwa na
Wakili Hashim Ngole za kudai waleta maombi hayo walikuwa  wazembe na walichelewa siku nne kuwasilisha Notisi baada ya rufaa yao kuondolewa na Jaji Fatuma Masengi  Desemba 2 hazina mashiko.

Jaji Opiyo, amesema  siku nne zinazolalamikiwa kuwa walichelewa kutoa maombi hayo, mahakama inaona hoja hizo hazina mashiko sababu siku mbili kati ya hizo zilikuwa siku za mapumziko jumamosi na Jumapili, hivyo walitumia siku mbili kuandaa nyaraka na kupeleka maombi hayo.
Akiwasilisha hoja za maombi ya kuongezewa muda wa kuwasilisha notisi hiyo ili rufaa hiyo iweze kusikilizwa Wakili Mfinanga alidai
mahakamani hapo kuwa maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo chini ya kifungu 361(2) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Alidai kuwa maamuzi wanayotarajia kukatia rufaa ni  uamuzi uliotolewa
 
Novemba 11  mwaka huu katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na  Hakimu Desderi Kamugisha, ambapo Lema anakabiliwa na kesi namba 440 na 441 za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

No comments: