Viongozi mbalimbali kutoka Hawza Imam Jafar Swadiq chini ya Sheikh Hemed Jalala na Kutoka Bilal Muslim Mission of Tanzania Sayyed Arif wakiongoza matembezi ya amani. |
Tukio la kufishwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) mbele
ya jamii ni jambo geni sana, kana kwamba katika historia ya ulimwengu tukio
hili halikutokea. Ingawa tukio la kuzaliwa kwa Mtume Muhammad limepokelewa kwa
nafasi kubwa isiyo kifani.
Kwa hiyo, unaweza kuona hafla mbalimbali za
kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) zikifanywa
Misikitini, Madrasani, Majumbani, na katika Mazawia mbalimbali.
Hili ni jambo jema sana, swali liliopo hapa ni,
je, huyu afanyiwae haya yu hai mpaka sasa? Au amekwisha kufa? Ni kwamba Mtume
Muhammad (s.a.w.w) amekwisha kufa.
Ndio maana katika mwezi huu wa Safar Waislam
katika maeneo mbalimbali duniani wamo katika huzuni na simanzi kubwa ya
kukumbuka tukio la kufariki dunia Mtume wa rehema, Muhammad (s.a.w.w).
Hapa Tanzania Uongozi
wa Chuo Cha Imamu Jafar Swadiq Chini ya Sheikh Hemed Jalala Unaadhimisha
Maadhimisho ya Kumbukumbuka Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) Ambaye alifariki
dunia tarehe 28 Safar mwaka wa 11 Hijria katika mji mtakatifu wa Madina.
Uongozi Huo Unawataka
Waislam Wote kuungana Pamoja katika kukumbuka kifo cha mbora wa daraja bwana
Mtume Muhammad (s.a.w.w), ili kusadia kuishughulisha jamii ya kiislam katika
kukuza maadili na mafundisho sahihi aliyofundisha Mtume Muhammad.
Katika kukumbuka kifo
cha mtume uongozi umeandaa Matembezi ya Amani ambayo yataanzia Karibu na Msikiti wa Kichangani, Magomeni
Kichangani Hadi Viwanja Vya Pipo kilichopo Kigogo-Post Jijini Dar es
salaam.Yakiwa na Ujumbe “Mtume katuachia Vizito Viwili
Tushikamanenavyo”.
Uongozi unawataka
Masheikh na Walimu kuihamasisha jamii ya kiislamu kukumbuka matukio muhimu
yaliyotokea, ili kuimarisha umoja na mshikamano baina ya waislam na wasiokuwa
waislam katika kuishi kwa amani na maelewano.
Pia tunawataka Waislamu
wote kufuata mafundisho ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Ahlulbayt
(Watu maalum wa Nyumba ya Mtume) , ili tuweze kufikisha ujumbe sahihi
aliotuachia, katika kukuza dini na ushirikiano baina ya Waislamu na Wasiokuwa
Waislamu.
No comments:
Post a Comment