Monday, September 28, 2015

Iran: Saudi Arabia imehusika na maafa ya Mina

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kufutwa kazi baadhi ya maafisa wa serikali ya Saudi Arabia kuhusu maafa yaliyotokea Mina wakati wa ibada ya Hija, hakutoshi.
Waziri Abdul Ridha Rahman Fadhli amesema kufutwa kazi baadhi ya maafisa waliohusika na maafa ya Mina hakutoshi na kwamba viongozi wa serikali ya Saudia wanapaswa kukabiliana na suala hilo la sasa kimantiki, kisheria na kwa njia zinazofaa ili waweze kufidia makosa yao ya huko nyumba.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema kwa mujibu wa baadhi ya ripoti, nchi kadhaa zimeafikiana na Saudi Arabia kuzika maiti za mahujaji wao mjini Makka lakini Iran inaendeleza jitihada za kurejesha nchini mahujaji wake wote wakiwemo wale waliotoweka na waliojeruhiwa, na Saudi Arabia inalazimika kushirikiana na Jamhuri ya Kiislamu katika uwanja huo.
 Amesisitiza kuwa, kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini Ayatullah Ali Khamenei, Saudia inapaswa kukubali majukumu yake na kuuomba radhi Umma wa Kiislamu kutokana na maafa ya Mina na kuwachukulia hatua maafisa wote waliozembea katika maafa hayo.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa mahujaji 169 wa Iran wameaga dunia, 295 wametoweka na 45 wamejeruhiwa.chanzo irib

No comments: