Monday, September 5, 2016

Profesa Kitilla: Huruma ya marais waliotangulia imekuza vyama



Profesa Kitilla MkumboKigoma. Kukua na kustawi kwa vyama vya siasa kuanzia mfumo huo ulipoanzishwa mwaka 1992 hadi sasa, kumetokana na huruma ya marais waliotangulia kabla ya awamu iliyopo sasa.

Kauli hiyo ilitolewa na mtaalamu wa elimu na saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitilla Mkumbo alipozungumza na baadhi ya wakazi wa Mji wa Kigoma kupitia asasi ya Meza ya Duara ya Watanganyika iliyopo Soko la Mwanga mjini hapa.

Hata hivyo, Profesa Mkumbo alisema anapongeza kitendo cha Rais John Magufuli kuzuia maandamano na mikutano ya vyama vya siasa nchini, kwa vile jambo hilo litawazindua Watanzania kudai Katiba bora ya nchi itakayojenga misingi ya uwajibikaji kwa kila mmoja na kuheshimu sheria.

“Lazima tumpongeze Rais wetu kwa kuzuia mikutano, maandamano na ubabe wa baadhi ya vyama vya siasa, anasaidia sana kukomaza vyama. Kukua kwa vyama vya siasa kulitokana na roho nzuri za marais waliotangulia, lakini sheria za nchi hii ni mbovu,” alisema.chanzo.mwananchi

No comments: