Friday, January 8, 2016

Maelfu waandamana kuulani jinai za Aal Saud duniani

Maelfu waandamana kuulani jinai za Aal Saud dunianiMaelfu ya Waislamu katika nchi mbalimbali za duniani wamefanya maandamano makubwa ya kuulani jinai za utawala wa Saudi Arabia kufuatia utawala huo kumuua shahidi Shaikh Nimr Baqir al-Nimr, mwanazuoni mkubwa wa Kishia nchini humo.
Leo Waislamu nchini Iran walimiminika mabarabarani katika miji yote baada ya sala ya Ijumaa na kulaani jinai za Aal Saud katika eneo hili.

Waandamanaji hao sambamba na kusema kwa saudi kubwa: "Kifo kwa Marekani, kifo kwa Israel na kifo kwa Aal Saud," wamelaani vikali hatua zilizo dhidi ya binaadamu zinazofanywa na watawala wa Saudia katika eneo la Mashariki ya Kati hususan nchini Yemen, Syria na Iraq na kuutaja utawala huo kuwa ni kiini cha matatizo ya Waislamu duniani.

Mbali na Iran, maandamano makubwa kama hayo yamefanyika katika nchi mbalimbali ikiwemo Pakistan ambapo waandamanaji wamewalaani watawala wa Aal Saud, na kubeba mabango na picha za shahidi Sheikh Nimr Baqir al-Nimr. Aidha waandamanaji wamemtaja shahidi Sheikh Nimr kuwa mfano wa kuigwa na mwanamapambano mkubwa ambaye licha ya mashinikizo mbalimbali kutoka kwa utawala wa Saudia, hakurudi nyuma katika azma yake ya kutetea haki za raia wa nchi hiyo.

Wapakistan pia wameitaka serikali ya Islamabad kukata mara moja uhusiano wake na Saudia ambayo wameitaja kuwa ni nchi yenye utawala unaolea magaidi na kuwakandamiza Waislamu.chanzo irib

No comments: