Friday, January 8, 2016

SALAAM ZA PONGEZA KWA MAZAZI YA NABII ISSA AS, (YESU) KWA WAKRISTO WOTE.



Akitoa  salaam   za Krismas  na  Mwaka  Mpya kwa  wakristo wote  Duniani,,  katika  mkutano  na waandishi  wahabari  uliofanyika leo katika  Hawzat Imam Swadiq  Dar es slaam, Sheikh Hemed  Jalala amesema: sisi  kama waislaam, viongozi  wa dini, watanzania, kama wanaadam , tunayohaki  ya kuwapa mkono wa  kheri  ya  krismas   kwa kusema tupo pamoja  katika  kusheherekea mazazi  ya Issa  as, au  Yesu .
 
Sheikh Jalala amesema: sababu kubwa  iliyotufanya  kuwaita  vyombo  vya  habari  ni  kuwatangazia  kua: wakristo ni ndugu zetu, ndugu zetu katika  asili moja, sote  tunatokana na Baba mmoja  Adam (a.s) na Hawaa ( Eva).” Wakristo  na  waislaam  wote  baba yao  ni Adam na  mama  yao ni Hawa, kwanini  tusipongezane  wakati sisi  ni waasili  moja?  Tofauti  tulizo nazo  hazivunji  udugu huu  wa kiasili:   Mwenyezi  Mungu  (S.W)  amesema  katika  surat Hujurat : 

39-13  Enyi watu  hakika  ni mekuumbeni  kutokana na  mwana mke  mooja  na mwanamume  mmoja, natukawafanya  mataifa  na  makabila  ili mjuane, hakika  mbora wenu  ni mchaji  mungu sana. Sisi  ni ndugu  kwa kua  ni watu  wa  Imani,  sote tunaamini  mungu  mmoja japo kua kuna  tofauti ndogondogo, tunaamini  kua  ipo siku ya  mwisho , siku  ya  kuhesabiwa.

Tunaamin  vitabu  4: Vilivyoletwa  kwa mitume  kuja kuwaongoza watu.  Taurati aliyopewa  Nabii  Musa  (a.s)  Zabuur  aliyopewa  Nabii Daud (a.s), Injili  aliyopewa  Nabii Issa (a.s), (Yesu). Na  Qur aan  aliyopewa Mtume Muhammad  (s.a.w.w), ikiwa  wakristo  wanaamini  katika  Tourat, injili  na  Zabuur,  ni mahala  pake  kuwapongeza, kwa  ni watu  wa  kitabu, hata Qur aan  inawaita  kwa  majina  mazuri  , Enyi  watu  wa kitabu. 

Waislaam  wanawaangalia   wakristo kua ni  ndugu  zetu, wanzetu, wanaadam wenzetu na wala  si   maadui,  ndio  maana mtume  Muhammad  (s.a.w.w) aliishi nao  vizuri  makkat  na  madina ,na kuwekeana  nao  Makubaliano  ya  kuishi  kwa  Amani.”  kwahiyo  tunayo hakki  ya  kuwaambia  ndugu  zetu   wakristo  kua  tupo  pamoja  katika  sikukuu  hii  ya  kuzaliwa  kwa  Nabii  Issa  as,  (Yesu).  

Na kwa  kua  sisi kama  Watanzania  na  wadau  wa Amani ,Tunaamini  vikao  kama hivi   vinajenga  na  kuimarisha  umoja  huu  na  mshikamano kwa  viongozi  wa  dini  na  waumini  kwa ujumla,mungu  Ibariki  Tanzania, Mungu  Ibariki Afrika,, na  viongozi  mungu  awatie  nguvu na  afya  njema  katika  kuwahudumia  wananchi  wao, Ahsanteni  sana.

Katika Quran Mungu anasema “Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanao sema: Sisi ni Manasara. Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi” surat Maida aya 82.

Ewe Nabii! Tunakuhakikishia ya kwamba utaona hapana watu wanao kuchukia na kukubughudhi wewe na wanao kuamini kama Mayahudi na hawa wanao mshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada. Na utawakuta walio karibu mno nawe kwa mapenzi ni wafwasi wa Isa, walio jiita wenyewe "Manasara". Kwa sababu wamo miongoni mwao makasisi wanao ijua dini yao, na marahibu (mamonaki) wat'awa, wanao mcha Mola Mlezi, na kuwa wao hawana kiburi cha kuwazuia wasisikie Haki. 

(Na haya yameonakana kuwa Waislamu wengi duniani asili yao walikuwa Manasara, Wakristo. Wao wakisha pata fursa ya kuufahamu Uislamu huufuata, lakini ni wachache miongoni mwa Mayahudi walio silimu. Kinacho wazuia ni kiburi. Lakini walio silimu basi wamekuwa Waislamu wakubwa.)
Na Imam Ali (a.s) anasema Udugu udupo wa aina mbili moja ni Udugu wa kuwa nyinyi ni Dini moja yaani nyinyi nyote ni Waislam pili Nyinyi mnatkana na asili moja yaani sote ni binaadam baba yetu ni Nabii Adam na Mama yetu ni Hawa (Eva).
Mwisho katika kuonyesha umoja wetu tumeandaa kadi za pongezi rasmi kupitia Ofisi yangu zikiambatana na zawadi ndogo kwa baadhi ya makanisa ili wapokee kwa niaba ya waumini wao, tunawaomba wazichulie zawadi zetu ndogo kama ishara ya upendo, umoja, maelewano na amani baina yetu.

Mungu Ibariki Tanzania.
Imetolewa na
Sheikh Hemed Jalala,
Mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania. Pia ni Kiongozi Mkuu wa Chuo cha Kiislam cha Imam Swadiq

No comments: