Wimbi la chuki dhidi ya Waislamu na maeneo yao ya ibada limezidi kuongezeka nchini Ufaransa.
Gazeti la Ufaransa la Le Figaro limeinukuu polisi ya mji wa
Perpignan, kusini mwa nchi hiyo ikitangaza kuwa, vitendo vya chuki
vinavyoambatana na vitisho dhidi ya jamii ya Waiislamu vinaonekana
kuongezeka zaidi Ufaransa.
Kwa mujibu wa polisi ya mji huo, hivi karibuni kumezuka watu ambao
wamekuwa wakichora picha na maneno ya kukashifu dini ya Kiislamu na
wafuasi wa dini hiyo tukufu kwenye kuta za misikiti na hivyo kuwaweka
Waislamu katika hali ya wasi wasi.
Gazeti la Le Figaro limemnukuu Yannick Janas, kamanda wa polisi wa
eneo la Perpignan la kusini mwa Ufaransa, akisema kuwa, hivi karibuni
watu wasiojulikana walichora picha ya mtu aliyekatwa kichwa na mikono
kwenye kuta za msikiti mkuu wa mji huo na kwamba hivi sasa polisi
wameanzisha uchunguzi wa kuwabaini wahusika wa picha hizo.
Hujuma na chuki dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa ziiliibuka baada ya
mashambulizi ya kigaidi ya tarehe 7 Januari na tarehe 13 Novemba mwaka
jana wa 2015.chanzo irib
No comments:
Post a Comment