Picha na Philemon Solomon-Fullshangweblog
………………………………………………………..
IDARA
ya Habari Maelezo imetangaza rasmi upatikanaji wa picha ya Rais wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli kwa matumizi ya
maofisini.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Msaidizi wa
idara hiyo, Zamaradi Kawawa, alisema kila nakala ya picha hiyo bila
fremu itauzwa kwa Sh 15,000 pamoja na picha ya Baba wa Taifa itauzwa Sh
5000 katika ofisi hizo.
Alisema
picha ya Rauis na ile ya Baba wa Taifa zinatakiwa kutundikwa katika
ofisi zote za Serikali, Tasisi za umma, Mashirika na ofisi binafsi.
“Serikali
inatoa onyo kwa wale wote waliokuwa wakitundika picha ya Rais isiyo
rasmi, wanatakiwa wazitoe haraka na waje katika ofisi zetu wanunue picha
rasmi,” alisema Kawawa.
Aidha
alisema picha hizo zitauzwa katika ofisi za Wakala wa Huduma za Ununuzi
Serikalini (GPSA), ambazo zimesambaa nchi nzima, hivyo watu wa mikoani
watazipata katika Ofisi hizo.
Alipoulizwa
kuhusu picha hiyo kucheleweshwa Kawawa alisema ilichelewa kutokana na
picha iliyotolewa mwanzo kutokuwa na bora na kuwalazimu kurudia
kutengeneza nyingine ambayo kimsingi inaubora wa kuridhisha.
No comments:
Post a Comment