WAZIRI asiyekuwa na Wizara maalum Profesa Mark
Mwandosya (pichani)imeeleza ni mchafu na hafai kwenye nafasi ya Urais.(Mtadandao huu
unaripoti) anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Profesa
Mwandosya ambaye ni Mbunge wa Rungwe Mashariki ni
miongoni mwa Makada wa chama cha Mapinduzi CCM walijitokeza
na kutaka nafasi ya Urais ikiwemo kuchukua fomu na sasa yuko kwenye Mikoa mbali
mbali ya Tanzania Bara pamoja na Visiwani Zanzibar –
Akitafuta Udhamini imebanika ni
mtu ambaye anatajwa kuwa asifikiliwe kwenye nafasi hiyo kubwa ya nchi kutokana
na kukumbwa kashfa mbali mbali .
Miongoni
mwa Kashfa ambazo zinatajwa kummaliza Profesa mwandosya ni ile ya Ubinafsishaji
Shirika la Ndege (ATC)pindi alipokuwa Waziri Mawasiliano na Uchukuzi kwenye
Utawala wa Awamu ya Tatu wakati wa utawala wa Rais Benjamini Mkapa huku shirika hilo likiwa linauwezo wa
kijiendesha lenyewe na kubinafsishaji huo ikapeleka shirika hilo kufa.
Mbali
na Ubabe wake huo kwenye Shirika La ATC pia Mwandosya anatuhumiwa pia kubinafsisha
Shirika la Reli (TRC) wakati wa Ubinasfishaji huo ulioleta maneno mengi,ambapo
kwa mijubu wa wachambuzi wa Mambo wanasema Ubisfishaji wa Shirika hilo ulikuwa
wakurupuka na ulikuwa unamaslahi Binasfi ya Kiongozi huyo.
Vilevile Profesa Mwandosya wakati huo huo
akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi anatuhumiwa pia Kubinasfisha Kampuni ya
Wazawa ya Simu ya (TTCL) Kwa kampuni ya NSI Detecon na Celtel bila kufuata
vigezo ambapo mpaka sasa Shirika hilo lipo hoi na mda wowote litakufa kutokana
na kuhelemewa na madeni.
Profesa
Mwandosya wakati akitangaza nia ya Urais ndani ya CCM mkoani Mbeya
alijisifu na
kusema atapambana na Rushwa ambapo pia anaTuhumiwa kwa Kashfa nyengine
ni ile ya kusomeshewa Mwanae na watu waliouziwa kampuni kwa Bei ya
kutupwa jambo hilo ambalo liliandikwa
sana kwenye vyombo vya Habari kwenye miaka 2001 hadi 2005.
“Mimi nilipomsikia akisema yeye atapambana na Rushwa nilicheka sana mtu huyu alipokuwa Waziri wa Uchukuzi alifanya uchafu kama ule yaani mashirika yote ya Umma ameyabinasfisha ambayo yalikuwa bado yanafaa kuendeshwa na umma harafu anataka urais mimi nakwaambia huyu mtu ni hatari sana”ameeleza Said Ally mkazi wa Ilala.
No comments:
Post a Comment