Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran amesisitiza udharura wa kuungana na kushikamama
Waislamu dhidi ya mirengo hatari ya kigaidi.
Ayatullah Akbar Hashimi Rafsanjani ameashiria suala la kuweko mirengo
hatari ya kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati hususan huko Syria,
Iraq, Afghastan, Pakistan na nchi nyingine kadhaa na kueleza kuwa:
Kushikamana kwa Waislamu na kujizuia na uhasama na mashindano yasiyo na
mwelekeo ni moja kati ya njia nzuri za kupambana na mirengo hatari ya
ugaidi. Ayatullah Rafsanjani ameongeza kuwa:
Makundi hayo ya kufurutu
ada yanafanya ukatili mkubwa na tunashuhudia namna makundi hayo
yalivyouzidishia masaibu ulimwengu wa Kiislamu na kuchochea hitilafu za
kidini na migawanyiko kati ya wafuasi wa madhehebu mbalimbali za
Kiislamu. Chanzo IRIB
No comments:
Post a Comment